Jinsi ya kutayarisha Mbolea Vunde/ Mboji
Mbolea vunde hutengenezwa kwa kutengenezwa kwa kuchanganya matabaka tofauti tofauti ya masalia ya mazao. Kadri mazalia yanavyoozeshwa ndivyo huwa mbolea vunde. Kuna njia nyingi tofauti za kutengeneza mbolea vunde.
Hii ni njia moja wapo
1. Chimba shimo na tayarisha msingi kwa kutumia vitawi au mabua
2. Majani makavu huupa udongo kaboni na kuboresha mfumo/ mpangilio wa odongo
3. Nyunyiza maji kusaidia biwi kuoza
4. Samadi ktoka kwa wanyama mfano Ng'ombe, kuku, mbuzi au sungura huongeza rutuba
5. Udongo wa juu wenye rutuba kwa wadudu na chambo (minyoo na kwenye udongo)
7. Mimea ya kijani/ mbichi huongeza viutubisho
8. Nyunyizia jivu kwa ajili ya madini ya madini ya postashiamu na maji ili kusaidia biwi kuoza
9. Kufunika na majani hukinga na kufanya mbolea vunde iwe na unyevunyevu
10. Tumia pima joto kuangalia kuwa biwi linaoza
Jinsi ya Kutayarisha Msingi
- Tafuta sehemu yenye kivuli
-Chimba shimo kwaaajili ya mbolea vunde
-Tayarisha msingi kwa kutumia vitawi au mabua
Jinsi ya Kupanga matabaka
1. Majani makavu
a. Maji
b. Samadi
c. Udongo wa juu wenye rutuba
d. Mimea ya kijani/ Mibichi
e. Jivu
-Rudia kila tabaka mara 3 au 4 funika kwa udongo na nyasi kavu
Jinsi ya Kugeuza Biwi
- Baada ya wiki 3 geuza biwi tabaka kwa tabaka
- Hii husaidia mbolea vunde kuiva
- Geuza tena baada ya wiki 3
- Baada ya wiki nyingine 3, itakuwa tayari
Kwa nini Kutumia mbolea vunde?
- Inaongeza mavuno
- Ni mbolea ya bure ya kilimo hai
- Inawezesha kuudia kimatumizi mabaki ya viumbe hai
- Inawasaidia viumbe hai kwenye udongo
- Inaboresha muundo wa Udongo
-Inahifadhi viturubisho kwa muda mrefu
-Ina uwezo mkubwa wa kutunza maji
-Inaua wadudu na magonjwa katika udongo