Mtama ni zao la
chakula na biashara. Ni zao muhimu katika maeneo yanayokabiliwa na
ukame. Na pia sehemu ambazo udongo una rutuba ya wastani. Utafiti wa
zao hili umeweza kutoa teknolojia mbalimbali ambazo zinaweza kutumiwa
ili kuongza tija katika uzalishaji. Teknolojia hizi ziko kwenye uwezo
wa wakulima.
Utayarishaji wa
shamba
Tayarisha shamba ili udongo uwe laini kurahisisha uotaji. Kama
shamaba limelimwa na trekta inabidi lipigwe haro na ikiwa
imetayarishwa kwa jembe la mkono. Mabonge mabonge ya udongo
yanatakiwa yavunjwe.
Kiasi cha mbegu
Upandaji kwenye mistari pasipo kupunguzia kunahitaji kilo 7 hadi 8
kwa hekta na upandaji kwa mashine unahitaji kilo 8 hadi 10 kwa hekta
Upandaji
Unaweza kupanda kwenye vumbi kabla ya mvua kunyesha au wakati wa mvua
zinapoanza au wakati mvua zimenyesha za kutosha kina: kupanda kwenye
vumbi cm 5.0-6.0; kupanda kwenye udongo wenye unyevu 2.5-4.0 nafasi.
Sehemu za unyevu mwingi: 60cm-20cm (cm 60 kati ya mstari an mstari na
cm 20 kati ya shina na shina); Maeneo ya makame: cm75 x cm 20 au cm
90 x cm 30
Mbolea
Aina mbalimbali za mbolea na samadi zinatumika kuongeza ratiba ya
udongo.
Samadi; Inatakiwa isambazwe kwenye shamaba na kulimiwa chini au
iwekwe kwenye mistari na kuchangwa na udongo kabla ya kupanda. Kiasi
kilichopendekezwa ni kiasi cha 5-10 kwa hekta na iwekwe mwezi mmoja
kabla ya kupanda.
Mbolea
Kabla ya kupanda; mbolea aina ya DAP, 20:20:0, 23:23:0 katika kiwango
cha kg 20 N na – 20 kilo P205 kwa eka, iwekwe wakati wa kupanda na
kabla ya kupanda mbegu .
Top dressing: kilo 20 N za mbolea aina ya urea, CAN iwekwe pembeni ya
mimea na hakikisha kuna unyevu wa kutosha wa kuyeyusha mbolea vizuri
.
Palizi
Palizi lifanyike mara mbili. Palizi la kwanza lifanyike wiki 2-3
baada ya mbegu kuota. Dawa za kuua wadudu zinazoweza kutumika ni laso
au gesaprim (kabla ya kuota) 2,4 D (baada ya kuota)
Kupunguzia
Mimea ipunguziwe ikiwa na wiki 3-4 baada ya kuota na ipunguziwe
wakati udongo una unyevu wa kutosha kupunguza madhaa kwa mimea.
Ukame na aina ya
udongo
Ukame ni moja wapo ya madhara makubwa yanadhuru mtama unaotegemea
mvua. Ukame unaweza kutokea kabla au baada ya kuchanua. Madhara ya
ukame yanaweza kuepukwa kwa kupanda mapema na kupanda mapema mapema
aina ya mbegu zinazowahi au kuvumilia ukame au kutumia mbinu
mbalimbali za kuifadhi maji.
Wadudu waharibifu
I) Inzi wa bua (Atherigona soccata), Madhara yanatokea siku 7 hadi 30
baada ya kuota. Viluwiluwi wanakula ndani ya mmea na kusababisha
dalili za moyo kufa (dead heart). Ucheleweshaji kupanda huongeza
madhara.
ii) Vitoboa -bua (sterm borers Chillo partellus), Dalili ni vidirisha
vidogo kwenye majani machanga, viluwiluwi hutoa bua na mimea michanga
inayoonyesha mioyo kufa (deadheart)