MADHARA YA MAZAO YALIYOBADILISHWA VINASABA KWA JAMII

Share:

Utangulizi
Mazao yaliyobadilishwa vinasaba (GMO) yamekuwa yakihamasishwa kulimwa katika nchi mbalimbali duniani. Hata hivyo, ulimaji wa mazao haya unaambatana na madhara mbalimbali ya kiuchumi, kijamii na kitamaduni ambayo hutokea katika jamii husika.

Madhara hayo ambayo husababishwa na matumizi ya mazao yaliyobadilishwa vinasaba hayajapewa kipaumbele ukilinganisha na yale yanayopewa kipaumbele ukilinganisha na yale yanayoweza kusababishwa na teknolojia husika. Hii ni kutokana na ukweli kwamba madhara ya kiuchumi na ya teknolojia yoyote ile yanachukua muda mrefu kuonekana, na yanapotokea yanakuwa yamekwisha sambaa kiasi ambacho inakuwa vigumu kuyadhibiti.

Kwa mfano, mazao yaliyobadilishwa vinasaba yanaweza kusababisha madhara ya kimazingira na kijamii ambayo hayawezi kubadilishwa (irreversible) kama vile uchafuzi unaofanywa na chavua. Pia, mazao yaliyobadilishwa vinasaba yana tabia za kipekee (unique) zinazofanya madhara yake kwa mazingira na kijamii kuwa makubwa na kusambaa zaidi.

A. Madhara ya Kiuchumi
Umiliki wa Nyanja za uzalishaji
Mazao yaliyobadilishwa vinasaba yanahusu umiliki wa mbegu na pembejeo zote zinazoambatana na uzalishaji wa mazao hayo ambao hautoi fursa sawa kwa wote. Hapa, swali muhimu la kujiuliza ni: Je, usambaji wa mbegu zilizobadilishwa vinasaba unatoa fursa kwa wakulima wadogo katika kumiliki pembejeo za kilimo, usindikaji na masoko?

Bei kubwa ya mbegu
Makampuni yanayotengeneza mazao yaliyobadilishwa vinasaba yanalenga kupata faida kwenye gharama walizowekeza katika utafiti na maendeleo ya  mazao hayo kupitia haki miliki za kitaaluma (interllectual property rights) na masoko pamoja na faida inayotokana na mauzo ya bidhaa zao. Mara nyingi bei ya mbegu zilizobadilishwa vinasaba inakuwa kubwa kuliko ile ya mbegu za kawaida kutokana na uwekezaji huo. Hali hii husababisha:
i. Wakulima wengi, hasa wenye kipato cha chini, kushindwa kumudu gharama kubwa za mbegu hizo.

ii. Makampuni yanayozalisha mbegu hizo huwalenga wakulima wenye kipato cha kati na kikubwa na kuwaacha wenye kipato cha chini.

Itaendelea..............