MADHARA YA ROUNDUP KATIKA UDHIBITI WA MAGUGU

Share:


Utangulizi
Udhibiti wa magugu ni changamoto inayowakabili wakulima wengi hapa nchini na kwingineko. Njia mbalimbali za kudhibiti magugu shambani hutumika zikiwemo kupalilia na kupulizia sumu. Mojawapo ya sumu zinazotumika kuua magugu ni ile ya Roundup na Weedall zenye kemikali ijulikanayo kama glyphosate.

Madhara ya matumizi ya sumu ya Roundup
. Sumu hii haichagui hivyo huua mimea yote inayokutana nayo shambani isipokuwa ile iliyobadilishwa vinasaba kutoa ukidhani dhidi yake.

. Huua wadudu muhimu ambao hufanya kazi ya kuongeza rutuba ya udongo

. Tafiti zilizonywa zinaonyesha kuwa sumu hii inaweza kusababisha kuota kwa magugu ambayo ni sugu dhidi ya sumu hiyo na hivyo kumuongezea mkulima gharama za uzalishaji

. Huchangia kuongezeka kwa magonjwa ya fungus (kuvu) kwa mimea