GMO ni aina ya mbegu na mimea ambayo imebadilishwa vinasaba (genes) katika maabara ili kuboresha aina fulani ya traits au tabia inayohitajika, kwa mfano kuongeza virutubisho, na kuongeza uwezo wa kujikinga na madawa.
Marekani ndio inaongoza kwa utengenezaji wa aina hii ya mbegu zikizambazwa na makampuni kama Monsanto, Syngenta AG, na DOW Chemicals ambazo nyingi tumekua tukiziona nchini. Hatari zitokanazo na aina hii ya mimea ni nyingi kuliko faida, na nchi nyingi duniani tayari zimezuia matumizi ya aina hii ya mbegu ikiwemo Canada, Argentina, Australia, India na Mexico na msimamo wa EU Ukiwa "Zuia GMO".
Faida chache alizonitajia ni pamoja na ongezeko la mimea inatojikinga na wadudu na magonjwa, kuongezeka kwa food supply, na kua na mimea inayostahimili ukame. Pia aliniambia "Hakuna Mwanasayansi duniani ambaye yuko serious atakayetoa support kwa GMO, UNLESS yuko katika payroll ya hayo makampuni", kwa sababu kiuhalisia, ni makampuni ya Biotech ambao ndio watengenezaji na wasambazaji watakaonufaika kutokana na mauzo ya mbegu na madawa!
Swali la kujiuliza; Je ni Watanzania wangapi wanazijua athari zitokanazo na GMO's?, au wengi wetu tumeangalia faida za kiuchumi kuliko athari za kimaziangira na kiafya?. TUAMKE NDUGU ZANGU!!