- Hakitumii mbolea na
madawa yenye kemikali sanisi
- Mifugo ya kilimo
hai haitumii viongezwa wala homoni
- Kinaongeza rutuba
ya udongo
- kinahusisha
matumizi asilia ya virutubisho
- Kinazuia ma
kudhibiti wadudu na magonjwa
- Hakihusishi
ubadilishwaji wa vinasaba (GMO)
- Kinatumia mbinu
nzui za asili na kitaalamu
KUNA FAIDA ZIPI
ZA KUNUNUA BIDHAA ZA KILIMO HAI
Chakula cha
kilimo hai ni kiafya zaidi ya kile kilichozalishwa kwa njia za
kutumia kemikali sanisi;
- Hakina mabaki ya
sumu yatokanayo na viuatilifu na mbolea zenye kemikali sanisi.
- Hakihusishi
ubadilishwaji wa vinasaba (GMO)
- Hakina homoni
zilizoongezwa
- Kina virutubisho
vingi na vya kutosha
Kilimo hai
kinatoa usalama wa chakula na kupunguza umasikini;
- Kinatoa njia endelevu na nafuu kwa wazalishaji wenye mtaji mdogo
- Maisha ya familia za wakulima wa kilimo hai yanaboreshwa kutokana
na bei nzuri ya bidhaa za kilimo hai katika masoko
- Kinapunguza utegemezi wa pembejeo pia kinajenga rutuba endelevu
katika udongo na kuongeza kiwango cha mavuno
- Kinajenga uwezo wa mzalishaji namna ya kutumia rasilimali alizonazo
- Rasilimali zitumikazo kusaidia mfumo wa uzalishaji wa kilimo hai
hupatikana katika mazingira yanayomzunguka mkulima
Kilimo hai
kinachangia kuboresha ustawi wa mazingira;
- Kinazuia mmomonyoko wa udongo na kupunguza kasi ya mazingia kugeuka
jangwa
- Kinachangia katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi
- Kinaongeza uwezo wa udongo kutunza maji
- Kinazuia uchafuzi wa vyanzo vya maji kwa kutoruhusu matumizi ya
pembejeo zenye kemikali sanisi
- Kinadumisha nasaba mbalimbali na ustawi wa viumbe kwa kuleta uwiano
wa kibio-anuwai katika mazingira
- Kinakataza matumizi ya moto katika kuandaa mashamba
Nini maana ya
alama ya Kilimo Hai
Matumizi kwa vitendo ya kilimo hai katika Afrika mashariki yanafuata
viwango rasmi vya mazao ya kilimo hai vya Afrika mashariki katika
soko la wakulima au duka la kilimo hai unasaidia kuendeleza ustawi wa
bio-anuwai katika uzalishaji wa kilimo hai kwa kula chakula
kilichozalishwa katika mashamba endelevu ya kilimo hai, unakuwa
umefanya uchaguzi sahihi kwa ajili ya familia yako na kuwasaidia
wakulima wa kawaida katika jamii yako.