Utunzaji wa udongo unategemeana kwa kiasi kikubwa na mazingira ya
kibiolojia. Kazi kubwa ya baadhi ya viumbe hai waliomo kwenye udongo,
ni kumeng’enya mabaki ya mimea na viumbe hai wengine. Mtiririko huu
hufanya uwepo wa nguvu, virutubisho, na hewa ya kaboni, ambavyo kwa
pamoja hutengeneza rutuba kwenye udongo.
Utunzaji wa rutuba ya udongo unaongozwa na filosofia hii ‘Lisha
udongo ili nao ulishe mimea.’ Udongo wenye rutuba utazalisha mimea
yenye afya inayoweza kukabiliana na magonjwa. Uzalishaji wa mazao kwa
njia za asili uhakikisha kunakuwepo uzalishaji wa kutosha bila ya
kutumia pembejeo za ziada isipokuwa matandazo, mboji na bila kutifua
udongo mara kwa mara. Ongezeko la malighafi za asili husaidia
kuimarisha udongo na kufanya kuwepo kwa virutubisho vya kutosha.
Athari kwa afya ya mimea
Kwa bahati mbaya, aina ya kilimo cha kisasa na kinachotumia
kemikali hufanywa tofauti na ilivyo kwa kilimo hai. Katika aina hii
ya kilimo; udongo hulimwa mara kwa mara jambo linalosababisha
uharibifu wa muundo wa udongo, uwiano wa virutubisho, ambapo
virutubisho huongezwa kwa kutumia mbolea za viwandani na matandazo
hayazingatiwi. Muundo wa udongo unapobadilika, rutuba nayo hupungua,
uwezo wa udongo kwenye udongo pia hupungua.
Kiwango cha udongo mzuri pia hupungua kwa kuwa hakuna tena viumbe
hai wanaotengeneza udongo ila unapungua kila msimu wa mavuno. Kwa
asili mzunguko huu huwa na matokeo yanayoishia kwenye afya ya mimea,
na hapa wadudu huchukua nafasi inayowawezesha kufikia malengo yao.
Ziba pengo
Wakulima wanatakiwa kuhakikisha kuwa kuna virutubisho vya kutosha
shambani mwao kila wakati. Ikiwa kuna mwanya pale ambapo baadhi ya
pembejeo zinakosekana, kununua virutubisho kwa ajili ya udongo
vilivyomo kwenye mfumo wa mbolea za asili inaruhusiwa. Hata hivyo,
weka utaratibu wa kuwa na virutubisho kutoka shambani mwako muda
wote.
Endapo tukitegemea kulisha udongo kutokana na mbolea za viwandani
na kutumia virutubisho vya asili, bado tutakuwa tunafanya sawa na
yanayofanyika katika kilimo cha kisasa. Tutakuwa hatujauongezea
udongo uwezo wa kujitengeneza na kuongezeka, jambo ambalo ndio msingi
muhimu wa kilimo hai.
Vyanzo vya virutubisho
Mimea inayofunika udongo
– Mimea inayotambaa huongeza na kushika virutubisho kwenye
udongo,kuongeza malighafi zinazooza kwenyeudongo, kuzuia madini ya
naitraitikuzama kwenye udongo, virutubishokutiririshwa, na mmomonyoko
waudongo. Jambo la muhimu hapa nikuwa udongo umefunikwa ili
kuzuiauharibifu. Mimea jamii ya mikundeinapendekezwa zaidi kwa kuwa
husaidia kuongeza nitrojeni kwenye udongo inayopatikana hewani.
Inashauriwa pia kuchanganya mimea jamii ya mikunde na nyasi kwa
kuwa nyasi hutumia nitrojeni nyingi sana kutoka kwenye udongo, hivyo
itasaidia kutokuharibika kwa mtiririko mzima wa uwekaji wa nitrojeni
kwenye udongo.
Mboji -
Mboji hasa inayotengenezwa kwa kutumia kinyesi cha wanyama, inaweza
kuwa chanzo kizuri cha viumbe wadogo kwenye udongo na virutubisho
vyenye gharama ndogo. Unapotumia mboji, changamoto kubwa ni
kuhakikisha kuwa imeoza vizuri na namna ya kuitumia kwa usahihi.
Endapo mchanganyiko uliotumika kutengeneza mboji hiyo yalikuwa na
ubora wa chini, basi mboji hiyo nayo itakuwa na ubora mdogo sana.
Itakuwa vizuri kama wakulima hawataacha mboji ikapigwa na jua au
mvua, kwa kuwa hali hii inaweza kusababisha kupotea kwa virutubisho
kwenye mboji. Kinyesi cha mifugo huboresha mboji zaidi.
Utafiti wa hivi karibuni unaonesha kuwa kiasi cha 15% ya
virutubisho vinavyopatikana kwenye mboji hutumika shambani kwa mwaka
wa kwanza. Hivyo, matumizi ya mara kwa mara ya mboji yanapendekezwa
ili kuweza kuongeza nitrojeni na malighafi zinazo oza kwenye udongo.
Samadi -
Samadi inayotokana na wanyama waliokomaa inaweza kuwa na uwiano mzuri
wa virutubisho vya nitrojeni na aina nyingine kwa kiasi kidogo.
Tatizo moja la samadi ni upatikanaji pamoja na kutokuwa na ubora
unaofanana wakati wote. Kiasi kikubwa cha samadi inayotumika kwenye
shamba la mboga, huozeshwa kabla ya kutumika, jambo linalosaidia
kupunguza madhara kwenye vyakula.