FAHAMU NAMNA YA KUZALISHAJI MBEGU BORA ZA MAHINDI

Share:
Mahindi ni zao linalolimwa karibu kanda zote za Tanzania. Zao hili hustawi vizurio zaidi katika maeneo yaliyo kati ya mita 0 – 2400 kutoka usawa wa bahari na hii inawezesha kuwa na aina nyingi za mahindi za muda mfupi, kati na mrefu

Mahindi ni chakula kikuu cha watanzania na huzalishwa sehemu nyingi hapa nchini, hivyo uzalishaji wa mbegu za mahindi ni muhimu katika kuboresha uzalishaji na tija katika kupata mavuno yaliyo bora.

Kila mzalishaji wa mbegu awe amepata mafunzo ya awali na kusajiliwa.

                                                       MAZINGIRA BORA

Hali ya hewa
. Mahindi hustawi vizuri eneo lenye wastani wa mvua wa mm 700 – 1800 kwa mwaka zenye mtawanyiko mzuri.
. Mahindi huota vizuri kwenye udongo unaopitisha maji
. Mahindi hustawi vizuri kwenye shamba lenye rutuba na linalotuamisha maji.

SIFA ZA SHAMBA
Historia ya shambani
Shamba ambalo halikulimwa mahindi msimu uliopita linafaa kwa uzalishaji mbegu za mahindi iwapo unataka kulima mahindi katika eneo lilelile unaweza kutukia mbegu za aina ile ile.
Utengaji wa shamba la mbegu
Tenga shamba lako kutoka kwenye aina na daraja lingine la mahindi mita 190 pande zote kutoka kwenye shamba lingine la mahindi. Tenganisha kwa muda wa siku thelathini (30) ukizingatia aina ya mbegu ya mahindi.

Sifa za ziada
Zingatia ubadilishaji wa mazao katika shamba lako; usipande zao lamahindi kwa muda wa misimu miwili ya uzalishaji. Kabla hujarudishia mahindi katika shamba lako panda mzao ya mikunde. Shamba lako lamahindi lisiwe na historia ya gugu aina ya kiduha (striga).

Utayarishaji wa shamba
Ukiisha chagua eneo lako lima kwa kina, endapo majani au magugu ni mengi shambani, inakubidi ulime angalau mwezi mmoja kabla yaq kupanda ili majani yaoze vizuri. Iwapo shamba lako ni la zamani lima kwa kina na lainisha udongo ili kiruhusu maji kupenya ardhini.

Chanzo cha mbegu
Mbegu zinakazotumika katika uzalishaji ziwe chotara. Mkulima atumie mbegu ya daraja la msingi, au kuthibitishwa ama QDS 1. Mbegu ya msingi na iliyothibitishwa hupatikana katika mashamba ya wakala wa mbegu za kilimo (Agricultural Seed Agency). Vilevile mbegu za daraja la kuthibitishwa hupatikana katika makampuni ya mbegu, kupitia kwa wakala wao au maduka ya pembejeo.

Mkulima anaruhusiwa kututumia mbegu ya QDS 1 iliyopatikana kutoka kwa mkulima wa mbegu aliyesajiliwa na TOSCI, kama chanzo cha mbegu, lakini ajue ya kwamba, akishavuna hawezi kutumia kama mbegu tena.

Aina ya mbegu zinazopendekezwa na wizara ya kilimo ni staha, kilima, kito, katumani, TMV.1, TMV.2, Tuxpeno

Angalizo
Kwa mkulima anaenza kuzalisha mbegu, anashauiwa kutumia mbegu ya daraja la msingi.

                                                             UPANDAJI

Wakati wa kupanda
Kwa matokeo mazuri ya mavuno ya mbegu panda wakati wa mvua za mwaka (masika). Vile vile mkulima atambue muda wa kukomaa, na avune wakati mvua zinakwisha.

Kiasi cha mbegu
Tumia kilo 8 – 10 kwa ekari na kilo 20 – 25 kwa hekta.

Nafasi ya kupanda
Mahindi yanaweza kupandwa kwa kutumia nafasi zifuatazo
i) sm 75 x 30 (tumia mbegu mbili) katika shimo na ng'oa bakiza mche mmoja baada ya kuota.
ii) sm 75 x 60 (mbegu tatu) kwa shimo, ng'oa moja bakiza mbili.

Matumizi ya mbolea
. Rutubisha udongo kwa kutumia samadi iliyoboreshwa au mboji
. Mbolea za kukuzia ni: chai ya samadi na chai ya mmea

Kusajili shamba la mbegu
Mara baada ya kupanda, mzalishaji analazimika kusajili shamba lake katika Taasisi ya udhibiti wa ubora wa mbegu (TOSCI) aidha katika kituo cha morogoro, Njombe au Arusha au sehemu au sehemu nyingine ambazo taasisi hiyo ina ofisi katika muda usiozidi siku 30 ili kutoa nafasi wakaguzi hao kupanga utaratibu wa ukaguzi.

                                                                     Palizi

Palilia shamba lako la mbegu ya mahindi mapema na hakikisha shamba lako linabaki safi wakati wote

Magugu hatari
Magugu hupunguza mavuno, hivyo ni muhimu kupalilia mapema, pia shamba lako la mbegu lisiwe na historia ya gugu aina ya kiduha (striga)

Kung'oa mimea isiyofaa na yenye ugonjwa
Ondoa mimea yenye magonjwa na iliyoharibiwa na wadudu, pia ondoa machipukizi,

Zingatia
Shughuli hii lazima ifanywe kwa kushirikiana na afisa ugani aliye karibu nawe.

Udhibiti wa Magonjwa na Wadudu waharibifu
. Hakikisha kwamba mimea yote yenye virusi na milia (maize streak virus inaondolewa)
. hakikisha unaondoa na kufukia mazao yaliyo na fugwe (smut disease).


Udhibiti wa magonjwa na wadudu waharibifu
. Hakikisha kwamba mimea yote yenye virusi wa milia (maize streak virus inaondolewa.
. Hakikisha unaondoa na kufukia mazao yaliyo na fugwe (smut disease)

Wadudu Waharibifu
. Fanya ukaguzi wa mara kwa mara ili kuangalia viwavi jeshi na kuwadhibiti kwa kutumia madawa yanayoshauriwa na wataalam wa ugani ambayo yanakubalika katika mbinu za kilimo hai.
.Tumia dawa za kuzuia Sondo, kwa kutumia viatilifu vya asili.
I
Wanyama Waharibifu
. Zuia wanyama waharibifu kwa kulinda, motego na kuwaarifu maafisa wanyama pori.

Ukaguzi wa Shamba la Mbegu
Ili kuhakikisha kuwa taratibu zote zinazotakiwa kufuatwa kwa ajili ya kuzalisha mbegu za kilimo hai zimezingatiwa, shamba la mbegu lazima likaguliwe, Ukaguzi wa ndani unafanywa na wataalamu husika kutoka miongoni mwa wanakikundi. Ukaguzi wa nje unafanywa na shirika la kilimo hai Tanzania na wataalamu kutoka taasisi ya kudhibiti ubora wa mbegu (TOSCI). Wataalamu wa TOSCI wanakagua shamba la mbegu mara tatu kabla ya kuchanua, wakati wa kuchanua na kabla ya kuvuna.

Uvunaji wa mbegu
. Mazao yavunwe mara baada ya ukaguzi wa mwisho.
. Vuna mahindi yaliyokomaa na kukauka vizuri mbegu zinazovunwa mapema mno hazizalishi mimea yenye afya. Dalili za mbegu ya mahindi kukomaa, kuonekana na doa jeusi kwenye gunzi.

Namna ya Kuvuna
Kuna namna mbili kuu za kuvun:
. kwenye mahindi; menya na kuweka kwenye mfuko
. Kata bua kutoka chini, halafu simamisha shambani kuelekea upepo utakapo

Ukaushaji
Kausha mbegu zako katika kichanja chenye paa kuzuia jua. Kausha mbegu kwa kupanga mabua kwa kusimamisha na yapange mithali na nyumba ya mmgongo punda

Uchambuzi wa mbegu
Chambua mahindi katika sehemu safi, ondoa yenye matatizo kama magonjwa, yasiyo komaa na yaliyopoteza sifa za mahindi na weka mbali mahindi yasiyo na sifa.

Kupukuchua
Pukuchua mbegu ya mahindi kutokana na nzi uliyoyachagua kama mbegu, usichukie mahindi yaliyoanguka au usichanganye mahindi yaliyoanguka ili kuhakikisha mbegu imekauka vizuri; jaribu kwa kung'ata kwa meno iwapo utasikia mlio tambua mbegu haijakauka vizuri.

Kuna aina tatu za kupukuchua:
. Kwa kutumia mkono
. Kwa kutumia mashine.
. Kwa kupiga kwenye gunia

Njia nzuri ni ya kutumia mkono ijapo kuwa huchukuwa muda mrefu, lakini ni salama zaidi kwani mbegu hazivunjiki.

Kupeta
Peta kwa kutumia ungo; ama kwa kutumia upepo.

Kuhifadhi mbegu
. Sehemu ya kuhifadhi iwe safi.
. Kihenge au ngoko kiwe kinazuia panya kuharibu mbegu.
. Chumba cha kutunzia mbegu kiwe kinapitisha hewa kwa urahisi. Pata ushauri wa wataalamu wa kilimo hai katika matumizi ya mbinu/ madawa ya asili kwa ajili ya kuhifadhi mbegu.

Vifaa vya kuhidhia mbegu
. Tumia vifaa safi, kama vile magunia, na mifuko au madebe.
.Panhga magunia yasigusane na ukuta na sakafu ili kuruhusu mzunguko wa hewa na ukaguzi.


. Weka utambulisho katika kila kifaa kilichowekwa mbegu.