Bilinganya
imo katika jamii ya mimea inayohusisha nyanya, pilipili, viazi
mviringo na nyanya mshumaa. Mboga hii ina viini lishe muhimu kama
vile madini aina ya chokaa na chuma, Vitamini A, B na C, wanga,
rotini na maji. Mboga hii hutumika kutengeneza supu au kama kiungo
katika vyakula mbalimbali.
Vilevile
huweza kuhfadhiliwa kwa kukatakata vipande na kuwekwa kwenye makopo.
HALI YA
HEWA
Zao hili
huhitaji hali ya joto la wastani, udongo wenye kina kirefu na rutuba
ya kutosha na usiotuamisha maji. Kwa kawaida bilinganya hulimwa zaidi
ya msimu mmoja, lakini katika nchi za kitropiki (joto) zao hili
hulimwa kwa msimu mmoja.
AINA
Aina za
bilinganya kwa wingi katika nchi za ukanda wa joto ni kama
zifuatazo:-
i) Black
Beauty:- Aina hii huzaa sana, matunda yake meusi, makubwa, na ya
mviringo
ii)
Florida Market:- Matunda ya Florida Market yana umbo la yai. Aina hii
pia huzaa sana, lakini hushambuliwa kwa urahisi na ugonjwa wa mnyauko
bakiteria (Bacterial wilt)
iii)
Florida High Bush:- Matunda yake ni makubwa yenye umbo la yai na
rangi ya kijani kibichi iliyochanganyika na nyeusi
iv)
Newyork Spineless:- Matunda ya Newyork Spineless ni ya mviringo,
makubwa na yana angi ya zambarau.
v)
Peredeniya:- Aina hii huzaa sana, matunda yake ni makubwa kiasi na
yana umbo la yai.
Aina
zingine za bilinganya ni matale, Kopek na Rosita. Aina hizi huvumilia
sana mashambulizi ya ugonjwa wa mnyauko bacteria.
KUOTESHA
MBEGU
Mbegu
huoteshwa kwanza kwenye kitalu na baadaye miche huhamishiwa shambani.
Kabla ya kusia mbegu, tengeneza tuta lenye upana wa mita moja na
urefu wowote. Weka mbolea za asili kama vile samadi au takataka
zilizooza vizuri, kiasi cha ndoo moja au mbili katika eneo la mita
mraba moja. Sia mbegu kiasi cha gramu mbili mpaka tatu (nusu kijiko
cha chai chenye ujazo wa gramu tano) katika eneo hilo.
Gramu
500 za mbegu zinatosha kupandikiza katika eneo la hekta moja. Nafasi
kati ya mstari na mstari iwe sentimeta 10 hadi 15 na kina kiwe
sentimita 1.5. Baada ya kusia mbegu fukia na tandaza nyasi kavu na
kisha mwagilia maji. Endelea kumwagilia kitalu kila siku, asubuhi na
jioni, hadi mbegu zitakapoota. Mbegu huota baada ya siku ya 10 hadi
12.
KUHAMISHA
MICHE
Miche
huwa tayari kwa kupandikizwa shambani baada ya wiki sita hadi nane.
Wakati huu huwa na urefu wa sentimita 15 mpaka 20 (sawa na urefu wa
kalamu ya risasi).
Mwezi
mmoja kabla kupanda miche, rutubisha udongo kwa kuweka mbolea za
asili zilizooza vizuri. Mbolea hizi ni kama samadi, mbolea vunde na
mbolea ya kuku.
Weka
kiasi cha tani 10 hadi 20 kwa hekta. Kiasi hiki ni sawa na kuweka
ndoo moja hadi mbili zenye ujazo wa lita 20 katika eneo la mita mraba
moja. Mbolea ya mchanganyiko aina ya N.P.K yenye uwiano wa 20:10:10
huwekwa kwenye shimo wakati wa kupandikiza mche. Kiasi
kinachohitajika ni gramu tatu hadi tano (sawa na nusu kijiko mpaka
kijiko kimoja kidogo cha chai) kwa kila shimo.
Nafasi
ya kupandikiza hutegemea aina ya bilinganya. Aina ndogo hupandikizwa
katika nafasi ya sentimita 80 mpaka 100 kutoka mstari hadi mstari na
sentimita 50 mpaka 60 kutoka mche hadi mche. Aina kubwa hupandikizwa
katika nafasi nafasi ya sentimita 80 mpaka 100 kutoka mstari hadi
mstari na sentimita 80 mpaka 90 kutoka mche hadi mche. Kazi ya
kuhamisha miche ifanyike kwa uangalifu mkubwa ili kuepuka kuikata
mizizi.
KUTUNZA
SHAMBA
Kuweka
matandazo
Mara
baada ya kupandikiza miche, tandaza nyasi kavu. Matandazo husaidia
kuhifadhi unyevu, huzuia magugu yasiote na huongeza rutuba ya udongo.
Palizi
Hakikisha
shamba ni safi wakati wote ili kuzuia ushindani wa chakula, maji na
mwanga kati ya mimea na magugu. Usafi wa shamba pia huondoa maficho
ya wadudu waharibifu na huzuia kuenea kwa magonjwa.
Mbolea
Mbolea
ya kukuzia aina ya S/A huwekwa wiki tatu baada ya mmea kuanza kutoa
maua. Kiasi cha gramu tatu hadi tano kuwekwa kuzungukia kila mche.
Mbolea iwekwe katika umbali wa sentimita tano mpaka 15 kutoka kwenye
shina, hutegemea ukubwa wa mche. Hakikisha mbolea haigusi mmea.
Kukata
Kilele
Wiki
mbili baada ya kupandikiza miche, kata sehemu ya juu ya mmea (kilele)
kama umepanda aina ndefu ya bilinganya. Hii itasaidia kupata matawi
matatu hadi manne na mmea kutengeneza kupata matawi matatu hadi manne
na mmmea kutengeneza umbile la kichaka. Matawi yakizidi manne
yaondolewe ili kupata mazao mengi na bora.
Kumwagilia
Zao
la bilinganya hustawi vizuri likipata maji ya kutosha. Umwagiliaji
ufanyike kila siku asubuhi na jioni kutegemea hali ya hewa.
WADUDU
WAHARIBIFU
Vivtatomvu
vya bilinganya
Wadudu
hawa hushambulia zaidi sehemu ya chini ya jani. Hufyonza utomvu wa
majani na kusababisha majani kuwa na mabaka meupe au njano.
Mashambulizi yakizidi majani huanguka chini.
Vidukari
au Wadudu mafuta
Hawa
ni wadudu wadogo wenye rangi nyeusi. Hushambulia majani machanga na
kuyasababisha kudumaa na kukunjamana.
Utiriri
wa mimea
Ni
vidudu vidogo vyenye rangi nyekundu iliyoiva. Hushambulia majani kwa
kufyonza utomvu. Majani yaliyoshambuliwa huonyesha utando kama wa
buibui. Mashambulizi yakizidi mea hudumaa, majani hukauka na hatimaye
hufa.
Minyoo
Fundo
Wadudu
hawa hushambulia mizizi. Hutoa kinyesi ambacho ni sumu kwa mmea. Sumu
hii husababisha mizizi kuwa na nundu kama ya mizizi ya maharagwe.
Mashambulizi yakizidi mmea hudumaa, hunyauka na hatimaye hufa.
MAGONJWA
Mnyauko
Bacteria
Ugonjwa
huu husababishwa na backteria. Mmea ulioshambuliwa hunyauka ghafla
hasa wakati wa jua kali.
Mnyauko bacteria unaweza kuziuwa kwa
kubadilisha mazao shambani. Endapo ardhi itashambuliwa na ugonjwa huu
zao la bilinganya lisipandwe katika eneo hilo kwa muda wa miaka
mitatu hadi mitano.
Njia
nyingine ni kupanda aina za bilinganya kama vile Matale, Kopek na
Rosita ambazo huvumilia mashambulizi ya ugonjwa huu.
Phomopsis
Vexans
Ugonjwa
huu husababishwa na bacteria na kushambulia majani, shina na matunda.
Verticillium
Wilt
Huenezwa
na maji na husababisha mmea kudumaa, majani kukunjamana na kuanguka.
Magonjwa
ya Phomopsis vexans na Verticillium Wilt yanaweza kuzuiwa kwa kung’oa
ma kuchoma moto mimea iliyoshambuliwa, kubadilisha mazao, na kuweka
shamba katika hali ya usafi wakati wote.
KUVUNA
Bilinganya
huanza kutoa matunda yaliyokomaa baada ya miezi miwili hadi mitatu
tangu kupandikiza. Uvunaji huendelea kwa muda wa zaidi ya miezi minne
na hauna budi ufanyike mapema mara matunda yanapokomaa. Matunda
yaliyokomaa sana hayafai kulimwa kwa sababu huwa na kambakamba na
mbegu zilizokomaa.
Vuna mara mbili au tatu kwa wiki, kwa kutumia
kisu kikali ili usiumize matunda.
MAVUNO
Kwa
kawaida zao hili huzaa sana iwapo limetunzwa vizuri. Shamba
lililotunzwa vizuri linaweza kutoa mavuno tani 50 hadi 60 kwa hekta.
Hata hivyo mavuno mengi hutegemea aina ya bilinganya, umwagiliaji na
rutuba ya udongo.
Mnyauko bacteria unaweza kuziuwa kwa kubadilisha mazao shambani. Endapo ardhi itashambuliwa na ugonjwa huu zao la bilinganya lisipandwe katika eneo hilo kwa muda wa miaka mitatu hadi mitano.
Vuna mara mbili au tatu kwa wiki, kwa kutumia kisu kikali ili usiumize matunda.