Boga
ni zao ambalo mmea wake unakuwa kwa kutambaa na ni la mviringo, ngozi
yake ni nyororo na rangi yake ni ya njano inayoelekea kwenye rangi ya
chungwa au rangi ya kijani. Katikati ya boga kuna mbegu na massa,
Boga lipo katika jamii ya
Cucurbita
pepo.
ASILI
YAKE
Asili
ya boga ni Amerika kaskazini, maboga yamekuwa yakipandwa kwaajili ya
biashara na kwaajili ya chakula. Kwa sasa maboga yamekuwa yakilimwa
maeneo mbalimbali duniani, Antarctika pekee ndiko maboga hayawezi
kustawi. Mataifa yanayozalisha maboga kwa wingi ni Marekani (USA),
Canada, Mexico, India, and China.
HALI
YA HEWA NA UDONGO
Maboga
yanahitaji joto la wastani kutoka kwenye jua, pia eneo ambalo
halituamishi maji udongo wake uwe na pH kati ya 6.0 – 6.8. Pia
udongo uwe na joto inchi tatu (sm 7.6) kushuka chini angalau nyuzi 60
°F (15.5 °C), maboga yatadhoofika kama maji
UTAYARISHAJI
WA SHAMBA
Shamba
litayalishwe kwa umakini bila kuwa na sehemu ya kutuamisha maji maana
mmea wa maboga na maboga yenyewe hutambaa chini, tumia jembe la
ng’ombe, trekta, jembe la mkono au pawatila, changanyia mbolea za
asili (samadi au mboji) na udongo ili kurutubisha shamba.
UTAYARISHAJI
WA MBEGU
Mbegu
za maboga zinatoka ndani ya maboga. Andaa mbegu mapema wiki moja au
mbili kabla ya kupanda.
UPANDAJI
Maboga
hupandwa kwa kufukia mbegu sentimita 1 au 2 chini ya udongo , panda
mbegu 2 kila shimo. Pia panda umbali wa sentimeta 30 kutoka shina
hadi shina na mita 1.5 – 2 kutoka mstari hadi mstari.
MATANDAZO
Kwasababu
ni zao linalotambaa basi lazima tuangalie namna ya kutandaza, weka
nyasi na mabaki ya mimea mingne kufunika ardhi. Baada ya miche
kutambaaa kwa kiasi unaweza kuweka matandazo (mulches) ambayo yaweza
kuwa nyasi kavu kwenye udongo ili kuzuia upotevu wa unyevu vile viile
kupunguza uotaji wa magugu shambani kwako. Vile vile matandazo
yakioza yanaongeza rutuba kwenye udongo na hulinda udongo dhidi ya
mmomonyoko wa udongo.
MBOLEA
Katika
matumizi ya mbolea yanatofautiana kutokana na mbegu, Lakini tumia
mbolea za asili (samadi au mboji) ili kuongeza rutuba kwenye udongo.
UPALILIAJI
NA UNYEVU
Palilia
shamba nyasi zinapoanza kuota, pia safisha shamba ili kuondoa wadudu.
Shamba la maboga linatakiwa liwe na unyevunyevu kila mara ili maboga
yaweze kustawi vizuri yasidumae.
UVUNAJI
Maboga
hukomaa baada ya siku 95 mpaka 120, ili kujua kuwa boga lako
limekomaa unaangalia kikonyo, kikonyo cha boga kinapoteza maji na
kinaanza kuwa kikavu.