FAHAMU KUHUSU UTUNZAJI ASILIA WA MAZAO

Share:

Utunzaji wa mazao ni utaratibu au shughuli ngumu inayohitaji kuelewa uhusiano uliopo kati ya mazingira, njia za kilimo na mfumo wa kilimo unaotumika zaidi.

Kwa hiyo utunzaji wa mazao hauwezi kuwa wa aina moja, bali unahitaji kuchanganya mbinu mbalimbali zinazofaa kwa kutegemea aina ya zao, hali ya hewa na sehemu. maarifa haya ni muhimu sana kwa mkulima kwani humsaidia kufanya uamuzi wa jinsi ya kutunza mazao au mimea yake.

Ni muhimu kuelewa kuwa njia za asili za kutunza mazao, ni moja tu kati ya mbinu mbalimbali. Hivyo ni muhimu kuchanganya mbinu hizo kutegemeana na aina ya zao na sehemu. Kwa ujumla matokeo ya mbinu za asili siyo ya papo kwa papo kama ilivyo kwa sumu za kuzuia au kuua wadudu za kemikali, lakini baada ya muda mrefu huleta faida au manufaa yafutayo:

. Kuondoa kabisa uwezekano na wadudu waharibifu kuwa sugu
. Kuwa na athari ndogo za uhaibifu wa maadui asilia wa wadudu wahaibifu
. Zinaondoa kabisa uwezekano wa ushambuliaji au kutokea tena kwa wadudu waharibifu wa mazao
. Hazina madhara na kama  yapo ni kidogo sana kwa afya za binadamu na mfugo
. Hulketa madhara kidogo au kutokuwa na madhara kabisa kwa mazingira au kwa maji yanayotumika.
.Huondoa kabisa haja ya mkulima kutegemea zaidi aina moja ya sumu ya kemiukali.
. Huwa na ghaama ndogo sana.