JE UNAFAHAMU KINGA DHIDI YA MAGONJWA MBALIMBALI KWENYE MWILI WAKO NI NANASI

Share:

Mwili unapokosa kinga imara, huwa katika hatari ya kushambuliwa na kila aina ya magonjwa kama vile majipu au uvimbe 
(Inflamatory diseases) na magonjwa mengine.

Ili uweze kupambana na magonjwa yanayosumbua mwili wako, nanasi ni moja kati ya matunda yenye vitamin nyingi na virutubisho vyenye uwezo wa kuupa kinga mwili wako dhidi ya magonjwa mbalimbali

Virutubisho vya Bromelain’ vinavyopatikana kwenye nanasi. Hulifanya tunda hili kuwa muhimu sana katika kujenga na kuimarisha kinga ya mwili.

Ulaji wa nanasi kila siku unakuwa unajikinga dhidi ya magonjwa mengi hususani ugonjwa wa kuwashwa, kuvimba koo, ugonjwa wa baridi yabisi (Arthritis) na ugonjwa wa gauti (Gout).

Ili upate kinga madhubuti dhidi ya magonjwa niliyotaja hapo juu,unashauriwa Usile nanasi pamoja na chakula kingine kwa wakati mmoja maana kwa kufanya hivyo, virutubisho vitafanya kazi nyingine tofauti na uliyokusudia.


Faida nyingine za kula nanasi ni kama zifuatavyo;
CHANZO CHA MADINI
Mbali ya kuwa ni chanzo kizuri cha vitamin C, nanasi pia ni chanzo kizuri cha madini aina ya ‘Manganese’ ambayo yanaaminika kuwa na uwezo wa kuboresha ufanisi wa vimeng’enyo mbalimbali vya mwili, vikiwemo vya kuzalisha nishati na kinga. Hali kadhalika tunda hili lina kiwango cha kutosha cha Vitamin B1 (Thiamine).

USAGAJI WA CHAKULA
Nanasi lina virutubisho vinavyouwezesha mfumo wa usagaji chakula tumboni kufanya kazi yake ipasavyo. Pindi mfumo huu unapowezeshwa kufanya kazi yake vizuri, mtu huweza kupata choo laini na kwa wakati kama inavyotakiwa.

KUIMARISHA NURU YA MACHO
Inawezekana karoti ikawa ndiyo inayojulikana na watu wengi kuwa na uwezo wa kuimarisha nuru ya macho lakini nanasi nalo lina uwezo mkubwa wa kuimarisha nuru ya macho. Utafiti unaonesha kuwa ulaji wa tunda hili na matunda mengine, kiasi cha milo mitatu kwa siku, kunaondoa hatari ya kupungua kwa nuru ya macho kwa asilimia 36 kwa watu wazima.

KINGA YA MWILI
Nanasi linaaminika pia kuwa miongoni mwa matunda yenye Vitamin C kwa wingi ambayo kazi yake ni kuupa mwili kinga dhidi ya ‘wavamizi’ mbalimbali (free radicals), ambao wanapoingia mwilini, kazi yao huwa ni kuharibu chembembe hai za mwili.

Kwa kuongezea, Vitamin C inaaminika kuwa na uwezo mkubwa wa kuimarisha mfumo wa kinga ya mwili. Mwili huwa na uwezo wa kujikinga dhidi ya magonjwa madogo madogo kama vile mafua, kikohozi, homa na maambukizi mengine.