Nyanya
Chungu ni zao la kitropic linalotoa mazao yake kama matunda na
kutumika kama mboga, kuna aina mbalimbali za nyanya chungu ambazo ni
nyanya chungu ambazo ni za asili na zingine ni chotara sio chungu
kama za asili. Rangi ya matunda huwa kijani kibichi au kijani-njano,
au njano-nyeupe, na yakipevuka kabisa hugeuka mekundu. Matunda
yafikia hatua ya kupevuka huwa hayafai tena kuliwa, ila kwa kutoa
mbegu za kupanda. Matunda hupikwa au kukaangwa na kufanywa mchuzi, au
huchanganywa na mboga zingine.
ASILI
YAKE
Nyanya
chungu asili yake ni Afrika Magharibi, lakini kwa sasa ime sambaa
Afrika ya kati na mashariki. Kutokana na ugunduzi wake Afrika
magharibi, zao hili pia linalimwa huko Visiwa vya Karibi, Amerika
kusini na baadhi ya maeneo ya kusini-magharibi mwa Asia. Nyanya
chungu hulimwa kwa matumizi ya chakula, matumizi ya dawa, na matumizi
ya mapambo.
HALI
YA HEWA
Nyanya
chungu za aina zote hustawi sana sehemu yenye jua na udongo
wenye kupitisha maji vizuri na udongo wenye pH kati ya 5.5 na
6.8. Gilo ni aina ambayo hustawi sana kwenye joto la mchana ni kati
ya 25°C na 35°C (77°F na 95°F). Kumba ni aina hustawi maeneo
yenye joto sana la 45°C na unyevu kidogo, Shum ni aina inahitaji
joto na unyevu ili kustawi. Hakuna aina ya Nyanya chungu inayovumilia
kwenye baridi kali na hali ya majimaji.
UTAYALISHAJI
WA SHAMBA
Lima
shamba lako vizuri kwa kutumia trekta, jembe la ng’ombe, jembe la
mkono au pawatila, hakikisha shamba linakuwa halina nyasi, changanya
samadi au mboji na udongo ili kuongeza rutuba.
UTAYALISHAJI
WA MBEGU
Mbegu
za nyanya chungu zinauzwa kutoka baadhi ya makampuni ila kuna njia ya
kupata mbegu kutoka kwenye tunda. Chukua nyanya chungu iliyokomaa
menya vizuri baada ya hapo kusanya mbegu zilizopo ndani ya tunda,
baada ya hapo ziweke kwenye kipande cha karatasi ili zikauke katika
sehemu isiyopitisha mionzi ya jua ya moja kwa moja. Mbegu zikisha
kauka zinaweza kutunzwa kwa miaka mingi na kuendelea kutumika. mbegu
lazima zioteshwe kwenye kitalu cha sentimita 15 (6 inch) au zaidi 20
cm (8 inch) ya safu. miche kutoka kitaluni inakuwa tayari kupandwa
ikifika urefu wa sentimita 15 mpaka 20 (6–8 inch) na iwe na majani
5–7. Mmea inatakiwa uwe na nguvu katika mashina na yenye nafasi ya
sentimita 50 (20 inch) mbali ruhusu sentimita 75 (30 inch) ya safu.
UPANDAJI
Kutoka
kwenye kitalu miche ifikiapo kimo cha sentimeta 15 hadi 20 au majani
manne 5-7 hupandikizwa bustanini , kwa umbali wa sentimita 50
kwa 75 au sentimeta 90 kwa 90, hadi 120 kwa 120; hii
kutegemeana na ukubwa wa kichaka chake. Mimea ya “Ngogwe”
hutunzwa kama bilinganya, huhitaji ardhi yenye rutuba na unyevu wa
kutosha. Mazao huanza kuvunwa miezi miwili baada ya kupandikizwa, na
uvunaji huendelea kwa muda mrefu kidogo.
MBOLEA
Zao
hili unashauriwa kutumia mbolea za asili (samadi au mboji kuongeza
uzalishaji wa mazao. mmea wa nyanya chungu unahitaji sana madini.
UPALILIAJI
& UNYEVU
Shamba
la nyanya chungu linatakiwa lipaliliwe kwa kuondoa nyasi na liwe safi
ili kudhibiti magonjwa na wadudu, unyevu unahitajika ili kuongeza
mavuno.
MAGONJWA
&WADUDU
Nyanya
chungu ni mmea mgumu, kwani unaweza kustahimili upungufu wa maji
kuliko aina nyingine za Mboga. Vile vile haushambuliwi sana na baadhi
ya Magonjwa
yasababishwayo na mvua au uchepechepe mkubwa. Ingawa yako magonjwa na wadudu ambao hushambulia zao hili, madhara yake si makubwa sana kiasi cha kutisha au kumkatisha tamaa mkulima. Usafi wa bustani na kubadilisha mpando wa mazao, vinaweza kuondoa tishio hilo.
yasababishwayo na mvua au uchepechepe mkubwa. Ingawa yako magonjwa na wadudu ambao hushambulia zao hili, madhara yake si makubwa sana kiasi cha kutisha au kumkatisha tamaa mkulima. Usafi wa bustani na kubadilisha mpando wa mazao, vinaweza kuondoa tishio hilo.
UVUNAJI
Nyanya
chungu huvunwa wakati zikiwa bado mbichi, hukomaa baada ya siku 100
mpaka 120 kutoka kupandwa, unashauriwa uvune kabla hazija badilika
rangi . Ili ziweze kukaa kwa muda mrefu (hata majuma mawili) bila
kuharibika, inapendekezwa kuzichuma pamoja na sehemu ya vikonyo
vyake. Vikonyo hivyo hukobolewa wakati wa kuzitayarisha kupikwa. Kwa
hiyo, zao hili linaweza kusafirishwa hadi masoko ya mbali bila
kuharibika.
SOKO
soko
la nyanya chungu linaonekana kuwa zuri maana wahitaji wake ni wengi,
ila fanya utafiti ili kujiridhisha soko lake.