Mambo ya kuzingatia katika kilimo cha bamia
- Hakikisha unatumia mbegu bora
- Panda kwa nafasi
- Mwagilia maji ya kutosha kulingana na hali ya hewa
- Palilia shamba vizuri
- Dhibiti magonjwa na wadudu waharibifu kwa wakati
- Vuna kwa wakati unaotakiwa
Jinsi yakupanda
Mbegu
mbili zipandwe kwenye shimo moja. Nafasi ya upandaji iwe ni sentimita
30 toka shimo hadi shimo na sentimita 50 toka mstari hadi mstari. Kwa
aina ya bamia zinazorefuka sana iwe sentimita 40 kati ya shimo na
shimo na sentimeta 70 kati ya mstari na mstari.
Namna ya Umwagiliaji
Kama
unyevu wa ardhi hautoshi, inapendekezwa kutumia mojawapo ya njia za
kumwagilia maji bustanini kulingana na hali ya hewa ya eneo husika.
Palizi
Hakikisha
shamba ni safi wakati wote kwa kuondoa magugu mara tu unapoona
yamejitokeza ili kuongeza uzaaji wa bamia.
Wadudu waharibifu
Wadudu
wanaoshambulia zao hili la bamia kama vile kimamba, funza wa vitumba
na
utitiri mwekundu. Dhibiti wadudu hawa kwa kufuata njia zinazopendekezwa na wataalamu wa kilimo Kwenye eneo lako.
utitiri mwekundu. Dhibiti wadudu hawa kwa kufuata njia zinazopendekezwa na wataalamu wa kilimo Kwenye eneo lako.
Magonjwa
Bamia
hushambuliwa na magonjwa kama ukungu, ubwiri poda na kunyauka
huathiri zao la bamia hivyo ni vyema kuzuia kwa kufuata mzunguko wa
mazao na kutumia dawa kulingana na ushauri wa wataalamu wa kilimo
eneo ulipo.