Ili kutekeleza
utunzaji asilia wa mazao ni muhimu sana kuelewa mbinu asilia za
kufanikisha kilimo. Kwa hali hiyo matukio ya majanga ya kushambuliwa
na wadudu wahaibifu yanaweza kupunguzwa na utumiaji wa hatua za
utunzaji wa mazao.
I) KUELEWA MFUMO WA
UHUSIANO WA VIUMBE NA MAZINGIRA YA KILIMO
. Aina za wadudu
waharibifu na wadudu waharibifu na wadudu wenye manufaa katika shamba
illolimwa na katika neo la jirani.
. Biologia ya wadudu
waharibifu. Magonjwa naa wadudu wenye manufaa (maumbile. Mzunguko wa
maish, tabia ya kuuzana, taabia za kula n.k).
. Utaratibu
unaojirudia wa wadudu katika msimu mbalimbali na kutegemea kwao hali
ya mazingira.
. Aina ya madhara
wakati wa mzunguko wa maisha ya wadudu yatakayosaidia katika mbinu
zaidi za kuwadhibiti vizuri.
. Msimu au hatua ya
ukuaji wa mmea shabani ambapo ni hatari zaidi kushambuliwa na wadudu.
. Mimea mingine
(inayolimwa au ya porini) inayowavutia wadudu maalumu waharibifu.
. Wadudu marafiki au
vimelea wanaoweza kutumiwa kuwala wadudu hao waharifu.
. Wadudu marafiki au
vimelea wanaoweza kutumiwa kuwala wadudu hao waharibifu.
ii) KILIMO
MCHANGANYIKO CHA AINA MBALIMBALI
Mazao ya aina
mbalimbali yanayolimwa sambamba na maua au mimea ya porini
yatasababisha mfumo wa aina tofauti utakaosaidia kuwepo kwa maskani
na chakula kwa aina mbalimbali za ndege, wadudu na wanyama watambao
(jamii ya mijusi); ambapo pia hupunguza aina fulani fulani ya wadudu
waharibifu wa mazao.
iii) HALI YA ARDHI
Maeneo yanayolimwa
kama vile miteremko mikali ya milima, maeneo yasiyofikia au
yaliyozungushwa mimea ni maskini mazuri kwa ndege, wadudu na wantyama
watambaao (jamii ya mijusi) wanaowinda wadudu waharibifu.
iv) KUBADILISHA
MAZAO NA KUCHANGANYA MAZAO
Madhumuni makubwa ya
kubadili maazao ni kutenganisha aina fulani ya wadudu waharibifu, wa
zao fulani; ambao kukosekana kwa zao hilo huwafanya wahame au kufa
kwa kipindi hicho. Hivyo ni vizuri kubadilisha mazao ambayo si ya
jamii moja; katika msimu unaofuata, yaani mazao yanayo shambuliwa
zaidi na mdudu fulani, sharti yabadilishwe na yale ambayo mdudu huyo
hayapendelei. Kwa mfano: ili kuzuia bungua wa mahindi; ni vizuri
baada ya kuvuna mahindi msimu unaofuata maharagwe yaoteshwe. Hali hii
huharibu mzunguko wa maisha ya bungua wa.
Ni vizuri pia
kuchanganya mazao ili kupunguza mashambulizi ya wadudu.
V.MATUKIO ASILIA
YANAYOJIRUDIA NA WAKATI MUAFAKA WA KUPANDA
Kuchagua wakati
muafaka wa kupanda kunaweza kupunguza mashambulizi. Kufahamu mzunguko
wa maisha ya wadudu na mahusiano yake katika mazao yanayo shambuliwa
humrahisishia mkulima kuchagua muda wa kupanda. Kutokana na hili
mkulima anaweza kupanda mapema au kuchelewa kupanda, ili kuepuka
kipindi ambacho wadudu huzaliana kwa wingi.
Kwa mfano: nyanya
zilizopandwa wakati wa kiangazi hazipati magonjwa ya ukungu kwani
hakuna maji yakuzidi kiasi yanayolowanisha majani ili kuwezesha
vimelea vya ukungu kuota.
VI. KUTIA MBOLEA NA
AFYA YA MIMEA
Mimea yenye afya
nzuri zaidi hustahimili athari iletwayo na magonjwa na wadudu
waharibifu na kutoa mavuno mengi. Mbolea huwa na wadudu marafiki
ambao hurutubisha ardhi.
VII. ULIMAJI ARDHI
Utifuaji wa ardhi
kwa jembe la kukokotwa na ng'ombe au trekta un alengo la kuuairisha
funza na hatua nyingine ya kukua kwa wadudu waharibifu waliobaki
ardhini au kwenye mabua ya mazao. Kwa kuwachimbua wataunguzwa na jua
na kulikuwa na wanyama au ndege. Mabaki ya mazao hufukiwa na hivyo
kukutana na viumbe wa ardhini na unyevunyevu ambao huyaozesha na
kurutubisha ardhi.
VIII. UTEUZI WA AINA
BORA YA MBEGU
Uteuzi wa aina ya
mbegu inayostahamili wadudu au magonjwa husababisha wadudu waharibifu
na magonjwa kushindwa kuzaliana.
IX. USAFI WA SHAMBA
Usafi wa shamba
husaidia kuharibu mzunguko wa maisha ya wadudu waharibifu, wadudu
waharibifu hukosa masikani.
X. KUPANDA KWA
NAFASI
Kupunguza kivuli,
kupunguza matawi, kuondoa maotea na kushikilia mimea kwa miti ili
isilale ardhini: Matendo yote haya husababisha mazingira yasiwe
mazuri kwa maendeleo ya vimelea vya magonjwa na wale wadudu
waharibifu wapendao kuishi kwenye hali ya kivuli.
XI. MASUALA YA
KIJAMII
Utunzaji wa mimea ni
jukumu la jamii nzima. Mkulima binafsi hawezi kamwe kuchukua hatua
zinazofaa kupambana na wadudu waharibifu wanaoenea sehemu kubwa
mwenyewe.
Hapa ni mahali
pazuri pa kufikiria kushirikiana na majirani ili kuchukua hatua ya
pamoja kukabiliana na janga la wadudu.