. Huongeza Kinga yako ya mwili hasa kupambana na magonjwa madogo kama mafua, na kikohozi kutokana na kuwa na vitamin C
. Husafisha Mfumo wako wa chakula, kuondoa sumu mwilini na kuzuia tumbo kujaa gesi mara kwa mara
. Huleta hewa safi kinywani. Ni Muhimu sana kwa watu wanaonuka midomo
. Hukuongezea uchangamfu na kufanya siku yako ianze vizuri sana
. Husaidia majeraha kupona kwa haraka kutokana na kuwa na ascorbic acid ya kutosha. Pia huimarisha mifupa
. Husaidia mmeng’enyo wa chakula utakachokula asubuhi au mchana kwa kuondoa vikwazo vyote vinavyoweza kuzuia umeng’enyaji wa chakula.
. Himarisha Ngozi yako, kuondoa makunyanzi na kukupa muonekano mzuri.
. Husaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza uzito kwani maji moto ya limao huyeyusha mafuta ya kutosha.
. Huyapa macho yako afya nzuri na kuimarisha kuona.
. Huondoa hali ya kuhitaji kahawa kila asubuhi ambayo si nzuri kiafya.