Tango husaidia kuzuia sunstroke au mapigo ya moyo pia husaidia katika mmengenyo wa chakula,na huwa na nguvu kubwa katika kusafisha tumbo na kuilinda ngozi.
Faida ya kutumia Tango
Matango husaidia katika kuujenga mwili na kuusafisha mirija na kibofu cha mkojo,na ni mazuri kwa tumbo na utumbo mkubwa.
Chembechembe za matango zinatumika katika kuondoa sumu nje kutoka katika sehemu ambapo mdudu ameuma.
Hutumika katika kusafisha damu na pia hutibu magonjwa yanayo wapata watoto wadogo na kuijenga ngozi kwa afya nzuri.
Ulaji kwa wingi matango husaidia katika kuyatibu macho kwa wale wanaosumbuliwa na ugonjwa wa macho.
Tango husaidia kusafisha na kuilinda figo