NAMNA YA KUJIHUSISHA NA KILIMO HAI CHA MAEMBE

Share:

MAEMBE HULIMWA KWA WINGI KATIKA MIKOA YA TABORA, PWANI, MTWARA, TANGA, MWANZA, MOROGORO NA MBEYA. UZALISHAJI WAKE NI WASTANI WA TANI 159,472 KWA MWAKA. 

MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA UZALISHAJI
CHAGUA AINA BORA YA KUPANDA KULINGANA NA MAHITAJI YA SOKO.MIEMBE YA KUUNGA PANDA UMBALI WA MITA 10 KWA 10  KWA ILE AMBAYO SI YA KUUNGA PANDA UMBALI WA MITA 15 KWA 15 KWA KILA MTI MMOJA 

DHIBITI MAGONJWA, WADUDU, NA MAGUGU
• FANYA UKAGUZI WA SHAMBA MARA KWA MARA ILI UWEZE KUDHIBITI WADUDU NA MAGONJWA YA MATUNDA KABLA MADHARA HAYAJAWA MAKUBWA
• DHIBITI WADUDU, MAGONJWA NA MAGUGU ILI KUPATA MAZAO BORA AMBAYO YATAPATA SOKO ZURI NA KUWEZA KUHIFADHIWA KWA MUDA MREFU.

• HAKIKISHA SHAMBA NI SAFI WAKATI WOTE ILI KUPATA MATUNDA BORA
MAANDALIZI KABLA YA KUVUNA

• SAFISHA SHAMBA ILI KURAHISISHA UVUNAJI NA USAFIRISHAJI SHAMBANI.

KUKAGUA SHAMBA KUONA MAEMBE KAMA YAMEKOMAA MAEMBE HUKOMAA KATIKA KIPINDI CHA MIEZI 4 HADI-6 TANGU KUTOA MAUA KUTEGEMEA HALI YA HEWA NA AINA


DALILI ZA MAEMBE YALIYOKOMAA
• MAEMBE HUNG’ARA
• KWA AINA NYINGINE RANGI YA KIJANI HUFIFIA NA KUANZA KUBADILIKA KUWA YA MANJANO.

KUVUNA
• KWA MIEMBE MIFUPI CHUMA MAEMBE PAMOJA NA KIKONYO CHAKE
• KWA MIEMBE MIREFU CHUMA KWA KUTUMIA KICHUMIO MAALUMU