UMUHIMU WA KULA NDIZI MBIVU KWA AFYA YAKO BINAFSI

Share:


Ndizi mbivu imejumuisha vitamin nyingi na madini,na utendaji mkubwa wanyuzinyuzi. Tunda hili ni zuri kwa magonjwa ya tumbo na matatizo ya ini,pamoja na kidonda cha homa ya tumbo. Ndizimbivu ni nzuri kwa chanzo cha vitamin B,kalisiamu na fosiforasi.
Ndizi mbivu inaongeza lishe kamili kwa watoto wadogo na kwa wagonjwa, pia kuongeza nishati mwilini

FAIDA YA KULA NDIZI MBIVU NI KAMA ZIFUATAZAZO
Homa ya manjano na homa ya matumbo.Ndizi mbivu iliyo pondwa pia na kijiko kimoja cha asali na kula mara mbili kwa siku chache.

Uchachu kwenye mdomo:Chemsha ndizi mbivu iliyopondwapondwa kwenye kikombe kimoja cha chai ya maziwa na kunywa mara mbili au mara tatu kwa siku.

Kifua kikuu:Ndizi pevu iliyo pondwapondwa pamoja na nusu kikombe cha maziwa yaliyoganda,kijiko cha chai kimoja cha asali na kikombe kimoja cha maji ya nazi na kunywa mara mbili kwa siku.

Kikohozi:Changanya robo kijiko cha chai na unga wa pilipili manga pia na ndizi mbivu iliyo pondwapondwa na kula mara mbili au mara tatu kwa siku.

Ukosefu wa choo,kwa ujumla udhaifu na vidonda vyam tumbo.Kwa kawaida chukua ndizi mbivu kila siku.