KUPANDA NDIZI KWA MBINU ZA KILIMO HAI
UTARATIBU WA USIMAMIZI WA BUSTANI YA NDIZI
Usimamizi sahihi huimarisha mimea na hupunguza kuenea kwa wadudu na magonjwa.
- Weka mazalia 3 hadi 4 kwa shina
- Ondoa majani ya zamani kwani yanaficha magonjwa
- Acha majani 8 hadi 10 wakati mgomba unabeba, na 4 wakati wa kuvuna
-Tumia majani yaliyoondolewa kama matandazo.
- Ondoa machipukizi dume ili ku-punguza kuenea kwa ugonjwa
UDHIBITI WA MAGONJWA NA WADUDU
Kilimo hai kinasisitiza kuzuia maambukizi na kuenea kwa wadudu na magonjwa.
- Tumia aina zinazohimili magonjwa
- Tumia vifaa safi kwa ajili ya kupanda
- Hakikisha usafi wa shamba
- Eneo kuzunguka shina lisiwe na kitu chochote.
- Ongeza rutuba ya udongo.
- Haribu mashamba yaliyojaa ugonjwa na usipande ndizi kwa mwaka 1 hadi 2.
KUBORESHA RUTUBA YA UDONGO
Hifadhi ya udongo na maji
- Jenga uzio na panda mazao ya kufunika ardhi kuzuia maji kupotea na mmomonyoko wa udongo.
- Tumia miti ya kivuli na matandazo kuhifadhi unyevu wa udongo
Mbolea za kilimo hai
- Tumia mboji katika kupanda miche mashimo
- Ongeza mbolea kwa juu kabla tu ya kuchanua
KILIMO MSETO CHA NDIZI NA UDHIBITI WA MAGUGU
Mfumo wa ghorofa
Ghorofa ya juu
- Tumia miti ya kivuli kukinga dhidi ya upepo na kudhalisha mbao
Ghorofa ya kati
- Panda miti ya matunda, kakao na kahawa kushamirisha uzalishaji wa ndizi
Ghorofa ya chini
- Panda mazao ya kila mwaka na
mazao ya mikunde yanayofunika
udongo.
- Kupalilia kwa muda stahiki huon-
doa ushindani wa magugu na
magonjwa.
UTUNZAJI SAHIHI BAADA YA KUVUNA NA UPATIKANAJI WA SOKO
- Hifadhi sahihi baada ya kuvuna huzuia ubora kupungua.
- Mazao bora ya kilimo hai yana soko kubwa nje ya nchi.
- Shirikianeni na wakulima wengine kupunguza gharama za uthibitisho