Nanasi
ni tunda la kitropiki, pia ni
chanzo kizuri cha vitamin A na B, pia inakiwango kingi tu cha vitamin
C pamoja na madini kama vile: patasiam, magnesiam, kalsiam, na madini
chuma.
Asili
ya nanasi inaaminika kuwa ni Brazil na Paraguay huko Amerika ya
Kusini. Hapa Tanzania, nanasi hulimwa zaidi maeneo ya Bagamoyo,
Kibaha (Pwani), Tanga, Mtwara, Lindi, Geita na Mwanza. Lakini pia
maeneo yote ya pwani ya Tanzania yanafaa kwa kilimo cha nanasi.
Hali
ya hewa inayofaa kwa ukuaji wa nanasi
Kilimo
cha nanasi kinapendelea hali ya hewa ya joto na husitawi vema katika
mwinuko kati ya mita 0-1750 kutoka usawa wa bahari. Mwinuko wa mita
1300 hadi 1750. Mahitaji ya joto ni kati ya nyuzi joto 18°C hadi
35°C.
Udongo
unaofaa kwa kilimo cha nanasi
Kwa
kilimo cha nanasi chachu (pH) ya udongo inayofaa ni 5.5 hadi 6.0, na
hustawi vizuri zaidi katika udongo tifutifu na udongo wenye kichanga
usiotuamisha maji. Ingawa nanasi huweza kustawi katika udongo wa aina
yoyote ile, udongo wa mfinyanzi haufai kwa kilimo cha nanasi.
Maandalizi
ya shamba
Lima
shamba kwa trekta, kwa ng’ombe ama kwa jembe la mkono kwa kina cha
sentimita 30 hadi 45. Shamba la nanasi unaweza kulilima kwa sesa
(flat-bed) au kwa matuta (furrows).
Kwa
sesa: chimba mashimo kwa nafasi ya sm.60 kati ya mistari,
sm. 30 kati ya miche na sm. 80 kati ya kila mistari miwili. Weka
mbolea kianzio katika kila shimo na upande, hakikisha shamba lina
unyevu wa kutosha kabla ya kupanda. Weka tani 10 hadi 15 za mbolea ya
kuku, weka pia viganja 2 vya mbolea ya zizi katika kila shimo.
Upandaji
wa mananasi
Zipo
aina mbali mbali za ‘mbegu’ (machipukizi/maotea) lakini yale
yanayochipua kutoka ardhini hufaa zaidi na hukomaa mapema. Chagua
machipukizi mazuri yenye umri mdogo na yenye kulingana kwa ukubwa.
Iweke miche kwenye kivuli kwa siku 3 kabla ya kuipandikiza iweze
kutoa mizizi haraka. Pandikiza mwanzoni mwa mvua za masika. Nafasi
iwe sm.60 kati ya mistari, sm. 30 kati ya miche na sm. 80 kati ya
mistari miwili. Pandikiza miche 50,000 katika hekta moja.
Palizi
Palilia
shamba mara kwa mara ili kuhakikisha shamba halina magugu. Katika
kilimo cha nanasi magugu hudhibitiwa kwa palizi ya jembe, kung’oa
kwa mkono ama matumizi ya viuagugu. Matumizi ya viuagugu hurahisisha
zaidi palizi ya nanasi ukizingatia kuwa nanasi huwa na miiba katika
ncha za majani yake ambazo huchubua ngozi endapo palizi za jembe
zitatumika. Njia nyingine ni matumizi ya matandazo (mulch) ya majani
au plastiki (plastic mulch) maalum kuzuia magugu.
Mahitaji
ya mbolea ya mananasi
Weka
mbolea ya NPK gramu 50 hadi 70 kwa kila mche wakati wa kupanda. Weka
tena gramu 85 kwa kila mche baada ya miezi 3 na pia miezi 3 baadae.
Wadudu
na Magonjwa yanayosumbua minanasi
Nanasi
ni zao lisilosumbuliwa na wadudu ama magonjwa mara nyingi. Hii ni
faida kubwa sana kwa wakulima wa nanasi! Hivyo endapo patatokea
mashambulizi ya wadudu na magonjwa, ushauri zaidi wa kitaalam
utafutwe kukabiliana na tatizo husika. Hakikisha unakagua shamba ili
kuzuia wadudu kama wataonekana.
Uvunaji
wa mananasi
Nanasi
huanza kutoa maua miezi 12 hadi 15 baada ya kupanda kutegemeana na
aina ya nanasi au maotea ya mbegu yaliyotumika, muda wa kupanda na
joto la mahali husika. Kwa kawaida nanasi hukomaa miezi 5 baada ya
kutoa maua, hivyo nanasi huchukua miezi 18 hadi 24 kukomaa/kuiva.
Katika kilimo cha nanasi, mimea ikitoa maua kwa nyakati tofauti
tofauti itasababisha kuvuna kidogo kidogo na kwa muda mrefu. Kwa
sababu hiyo ndio maana ni muhimu kupanda kwa wakati mmoja mbegu zenye
umri na ukubwa sawa.
Kwa
wanaofanya kilimo cha nanasi kibiashara (commercial pinapples
production) hutumia kemikali aina ya Ethrel (@ 100 ppm) mwezi mmoja
kabla ya kuanza kutoa maua ili mimea mingi iweze kutoa maua kwa
wakati mmoja, angalau 80% ya mimea yote.
Vuna
wakati kikonyo cha nanasi kimebadilika rangi kuwa njano ya dhahabu.
Kata kikonyo cha nanasi chenye urefu wa sm. 30 kikiwa kimeshikana na
nanasi na upunguzie majani ya kichungi chake.
Utunzaji
wa mananasi
Hifadhi
nanasi katika eneo lenye ubaridi huku kikonyo ch
ake
kikielekea juu. Hakikisha unauza nanasi mara tu au siku 2 hadi 3
baada ya kuvuna ili kutunza ubora wake.