FAIDA YA KUTUMIA YA PAPAI
matunda yana vitamin ambavyo ni muhimu katika mwili wa mwanadamu. vitamin hivyo kama A, B, C, D, E. Na miongoni mwa matunda ambayo yanapatikana vitamin hizo zote ni papai pekee.
Faida ya tunda la papai kwa afya ya binadamu ni kama zifuatazo;
KISUKARI
Inasemakana wanaosumbuliwa na kisukari wanashauriwa watumie mapapai kwa wingi kwani virutubisho vilivyo katika tunda hilo vinasaidia kutibu kisukari. Pia kwa wagonjwa wa athma pia wanashauriwa kutumia tunda hili.
VIDONDA
matumizi ya majani ya mpapai baada ya kuyaponda ponda kisha kuweka katika kidonda itasaidia kuponya haraka kidonda kilichopo kwenye mwili
Afya Njema
Inasemakana matumizi ya papai kila siku inasaidia afya ya mwili wa binadamu kuimarika
USAGAJI WA CHAKULA
Inashauriwa na wataalamu wa afya utumiaji wa papai mara kwa mara inasaidia epukana na matatizo ya kusaga chakula mwilini.