Nyanya
ni mmea wa familia Solanaceae,
ambao daima hutambaa na ambao hukuzwa kwa makusudi ya kutumiwa na
watu. Matunda yake yanaitwa nyanya.
Kwa aina nyingi sana nyanya huwa na rangi nyekundu pindi inapoiva,
nyingine zina rangi ya manjano au machungwa. Mnyanya huwa na urefu wa
mita 1-3 na huwa na shina laini ambalo mara nyingi hujibebelesha
kwenye mmea mwingine. Majani huwa na urefu wa sentimeta 1-25, na
petali 5-9 Majani ya shina la nyanya huwa na vinyweleo. Maua huwa na
upana was m 1-2, rangi ya manjano na majani matano na huvunwa kwa
mwaka mmoja. na K, potasiamu na nyuzinyuzi
Nyanya
zina aina mbalimbali za viasili vya kurutubisha na visivyorutubisha
vinavyohusiana na faida kadha wa kadha
za kiafya. Hii inajumuisha lycopene, vitamini C, A
na K, na K,
potasiamu na nyuzinyuzi
Faida
za nyanya kiafya za nyanya katika mwili ni kama zifuatazo
-Kuusaidia
mwili kudumisha viwango vya lehemu vyenye kuleta afya bora.
-Kuongeza
uzalishaji wa nishati
-Kuweka
katika hali ya kawaida kikemikali cha kusawazisha sukari ya damu
(insulin) na kuzuia ongezeko la uzito wa mwili linaloweza kuhatarisha
afya.
-Kuulinda
mwili dhidi ya uharibifu utokanao na chembechembe za maradhi na
kuukinga na uzee wa kabla ya wakati
-Kudumisha
mfumo wa kinga ya mwili, mfumo wa umeng’enyaji, kudumisha afya ya
viungo vya mwili na mifupa
-Kuweka
msukumo wa damu katika kiwango bora cha afya.