Ukashauji
wa mboga za majani ni njia ambayo inatumika sana maeneo ya vijijini
lakini si vibaya ikianza pia kutumika maeneo ya mijini kwani ni njia
nzuri sana. Kwa maneno mengine njia hii ni usindikaji wa mboga za
majani. Na moja kati faida kubwa ambayo utaipata mara baada ya
kukausha mboga hizi ni kwamba mboga hizi zinaweza kukaa kwa muda
mrefu hivyo kusaidia wakati wa mboga zinapokuwa hadimu.
Mambo
ya msingi ya kuzingatia wakati wa kukusha mboga za majani ni
ifuatavyo:
1. Chuma
mboga nyingi katika bustani yako. Hajalishi ni mboga za aina gani.
2. Hatua
inayofuata ikatekate vipande vidogo vidogo.
3. Baada
ya hapo chemsha katika maji ya moto. Lakini jambo la kuzingatia ni
kwamba chemsha mpaka ibadili rangi yake, isiwe katika hali ya
ukijani.
4. Mara
baada ya kuchemka na kujiridhisha kwamba imeiva vizuri. Epuka kisha
subiri kwa muda fulani mpaka ipoe vizuri.
5. Ikisha
poa vizuri chukua kitu ambacho kitakusaidia kuianika mboga hiyo
mpaka ikauke vizuri.
6. Mara
baada ya kukauka vizuri ni kwamba unaweza ukaiifadhi sehemu safi ili
ije kuliwa hapo baadae.