UMUHIMU WA JUISI YA MIWA KWA AFYA YA BINADAMU
Kunafaida nyingi za juisi ya miwa. Baadhi ya faida hizo ni kama zifuatazo;
Huepusha magonjwa ya ini.
Juisi ya miwa husaidia kulinda maini yasipate maambukizi. Hii ndo maana Madaktari hushauri matumizi ya juisi ya miwa kwa wingi.
Juisi ya miwa inauwezo mkubwa wa kuipatia miili nguvu kwa haraka na kukata kiu ya maji.
Hii ni kwa sababu juisi ya miwa ina sukari “sucrose” ambayo kazi yake
kuu ni kutengeneza nguvu mwilini. Kwahiyo wakati mwingine ukiwa na nguvu
au uchovu, badala ya kunywa vinywaji vya viwandani tafuta juisi ya
miwa.
Husaidia kulinda ngozi dhidi ya mogonjwa ya ngozi.
Juisi ya miwa husaidia katika kupambana na mabaka mabaka na kung’arisha
ngozi. Juisi ya miwa huweza kutumika kama ” face mask na scrub” kwa
kuipaka kwenye ngozi na hivyo kusaidia katika kuing’arisha na
kuiimarisha.
Hupunguza uwezrkano wa kupata ugonjwa wa kansa.
Juisi ya miwa ina kiwango kikubwa cha madini ya calcium, magnesium,
potassium, chuma n manganese. Madini haya yana uasili wa ualkali ambao
husaidia kupunguza uwezekano wa kupata kansa kama vile kansa ya Tezi
dume “Prostate cancer” na kansa ya maziwa “Breast Canser”
Huzuia meno kuoza.
Uchunguzi unaonyesha juisi ya miwa husaidia kuzuia meo kuoza na matatizo
ya kupumua kutokana na kuwa na kiasi kikubwa cha madini. Kwa hyo kama
unafikiria kwenda kwa daltari kung’arisha meno yako, kunywa juisi ya
miwa mara kwa mara.