Fahamu Faida ya Kunywa Kahawa

Share:

Kahawa ni zao la kibiashara na ni maarufu duniani kwa muda mrefu sana na kinywaji chake kinapendwa na watu wengi sana kwasababu kinamanufaa mengi ndani yake.

Faida ya kunywa kahawa ni kama zifuatazo 
Virutubisho muhimu
Kahawa ni kinywaji chenye virutubisho muhimu kwa ajili ya afya za miili yetu.Inaelezwa kuwa kikombe kimoja cha kahawa kina virutubisho vifuatavyo:
Riboflavin (Vitamini B2): 11%, Asidi ya Pantothenic (Vitamini B5): 6%,
Manganese na Potasiamu: 3%, Magnesiamu na Niacin (B3): 2%.
Hundoa msongo wa mawazo
Inasemekana unywaji wa vikombe vinne vya kahawa kila siku hupunguza msongo wa mawazo kwa kiasi kikubwa.
Huchangamsha mwili
Caffeine inayopatikana kwenye kahawa huuchangamsha ubongo na kuufanya mwili kuwa katika hali nzuri.
Hii ndiyo sababu watu wengi wenye kazi nyingi hupenda kunywa kahawa wakati wa kazi .
Utaishi muda mrefu
Watafiti wanaeleza kuwa hatari ya kifo hupungua kwa silimia 20 kwa wanaume na asilimia 26 kwa wanawake kwasababu kahawa huzuia maradhi mbalimbali na watu wanaokunywa kahawa huishi muda mrefu zaidi.
Huyeyusha Mafuta ya mwili
Utafiti mmoja uliofanyika ulibaini kuwa kahawa iliweza kusaidia kupunguza mafuta kwa watu wanene kwa asilimia 10 na kwa asilimia 29 kwa watu wembamba
Hulinda Ini
Tafiti zinaeleza kuwa kahawa hupunguza uwezo wa seli za ini kuwa makovu (cirrhosis) kwa asilimia 80. Maana uvimbe kwenye ini pamoja na tatizo la seli za ini husababisha makovu na kuathiri ini kwa kiasi kikubwa