Hali ya hewa
Jotolidi; Chinese au linastawi na kukua vizuri kwenye maeneo yenye jotolidi 18 °c hadi 27° c.
Udongo; chinese cabbage linakua vizuri kwenye udongo wa kichanga na wenye unyevunyevu wa kutosha PH; 5.5 hadi 7.6
Uandaji wa shamba
Udongo unatakiwa utifuliwe vizuri kwa kutumia jembe la mkono au machaku na chisel kabla ya kupanda na andaa shamba wiki 6 kabla ya kupanda.
Maandalizi ya kitalu
Kitalu kinatakiwa kiwe na upana wa mita 1 yani sentimita 100 na urefu wa mita 5 yani sentimita 500. Kitalu kitifuliwe vizuri na kiwe na kingo ili kuzuia maji kutoka nje ya kitalu. kisha panda mbegu kwenye kitalu kwa sm 15 hadi 20 mstari hadi msitari na panda mbegu sm 2 kati ya mbegu na mbegu na fukia sm 1 hadi 2.
Upandaji
chimba udongo sm 2 hadi 3 kwa kutumia jembe la mkono na panda nafasi ya 30 mstari hadi mstari na 30 mbegu hadi mbegu na fukia sm1 hadi 2 na baada ya hapo hamisha miche inapo fikia urefu was sm 5 ili utumie kupandikiza na kwa matokeo mazuri chagua miche yenye afya na isiwe na magonjwa.
Mbolea.
Kama unatumia mbolea ya ng’ombe, kuku na nguruwe tumia ndoo katika kila kitalu chenye mita 5
Palizi
Tumia jembe la mkono kupalilia magugu
Magonjwa na wadudu waharibifu
unashauriwa uweze kutumia mbolea ya kilimo hai na kila wakati unakumbuka kuondoa magugu pamoja na mimea yenye wadudu na pia weka shamba safi wakati.
Lakini kama utatokea ugonjwa wa Kuoza kwa mizizi unachotakiwa kufanya kuondoa mazao yaliyo athilika na ugonjwa huo.
Kuvuna
Chinese ukomaa baada ya miezi 2 hadi 4 saa zingine inategemea na aina mbegu uliyopanda, au hali ya hewa pia.