FAHAMU NAMNA YA KUJIHUSISHA NA KILIMO BORA CHA MBAAZI

Share:
Mbaazi ni moja kati ya mazao yanayo limwa kwa wingi nchini Tanzania 

Hali ya hewa
kilimo mbaazi kinafaa kilimwe kweye hali ya hewa ya nyuzi joto 18 hadi 38 sentigredi.ila sehemu za baradi mbaazi haiwezi kukua.

Mbaazi hustawi kwenye mvua ya milimita 600 hadi 1000,pia mbaazi hustawi kwa muda mfupi kwenye kiwango kidogo cha mvua ya milimita 250. Kwa mujibu wa wataalamu mbaazi haistawi kwenye usawa wa bahari.

Aina za Mbaazi

Mbaazi ya muda mfupi
Aina ya hii mbaazi huwa inaota na kukua ndani ya miezi 3 hadi 3 na nusu.


Sifa za mbaazi za muda mfupi
Aina hii ya mbaazi huwa inakuwa na ufupi wa mita moja hadi moja na nusu yenye mauwa mekundu inapoanza kuchanua upendelewa kulimwa au hulimwa katika ukanda wa kati na wa chini katika uhaba wa mvua kama vile maeneo ya pwani
Aina hii hazichanganywi na mahindi ,kwasababu inaweza kuhatarisha mazao yako ya mbaazi kwa kushambuliwa na wadudu maana huchanua wakati wa mvua tatizo hili hutokea  hasa ukanda wa kati na wa juu
Tofauti na aina zote za mbaazi aina hii haiasiliwi na na urefu au ufupi wa siku hivyo itachanua wakati wowote mara baada tu ya kupanda
Haina hii ya mbaazi haina ukinzani wa ugonjwa wa kunyauka
Mbaazi za muda wa kati
Hukomaa ndani ya muda wa miezi minne na nusu mpaka miezi sita baada ya kupandwa.
Sifa za mbaazi za muda wa kati
Aina hii ya mbaazi zina matawi mengi na ni fupi kulingana na mbaazi za muda mrefu.hazikomai zote kwa wakati mmoja humlazimu mzalishaji kuvuna zaidi ya mara moja ingawa mazao ya kwanza ni mengi kuliko mazao yanayofata.zinapendwa na kina mama kwa sababu ya mboga kwa jili ya mboga au enderefu kwa sababu huchanua tena mara zikipata maji.
Mbaazi za muda mrefu
Mbaazi hizi huchukua miezi sita mpaka saba shambani mpaka wakati wa kuvuna.
Aina hii ya mbaazi zina matawi machache na ni ndefu na ni nzuri sana kwa kilimo mseto. Unaweza kuvunwa katika msimu mmoja lakini mazao yanayopatikana baada ya msimu wa kwanza huwa madogo hivyo inashauriwa aina zipandwe upya kila mwaka
Aina hizi hustawi vizuri katika ukanda wa juu na kati wenye mvua za kutosha .

Utayarishaji wa shamba
- N’goa visiki pamoja na mabaki yote ya mimea kabla ya kulima
- Lainisha udongo kwa kupiga halo mbaazi zinavyoota huwa dhaifu sana na kama shamba halikuandaliwa vizuri magugu huota mapema kabla ya mbegu za mbaazi
MN y - Tayarisha matuta au makinga maji kama shamba lipo kwenye mteremko .

Namna ya kuotesha
Nafasi kutoka mstari hadi mstari hutegemea zao kuu linalopandwa .kilimo mseto na mahindi hutegemeana pia na aina za mbegu sentimita 90 mpaka 120 sentimita unashauliwa kutoka mstari hadi msatri 50 sm kutoka shimo hadi shimo acha mimea miwili kwa shimo
Panda mahindi yanayo komaa mapema ili yavunwe mapema na kutoa nafasi kwa mbaazi ili kuchanua na kutanuka
Tumia kilo 4 hadi 5 kwa hekari kutegemeana na ukubwa wa punje

 Upandaji
Mbaazi za mda mrefu panda kwa mistari kwa umbali wa sm150 kwa sm100
Mbaazi za muda wa kati panda kwa mstari wa sm100 kwa 60sentimita
Mbaazi panda kwa umbali wa nafasi sm90kwa 60sentimita