FAHAMU KWA UNDANI KUHUSU KILIMO CHA ROZELA

Share:
Rosella ni mmea wenye virutubisho vingi kama vitamini na madini ya chumvi chumvi. Hutumika kutengeneza juisi, jam, jellies, sauces na mvinyo(pombe). Rosella hutumika kama kinga ya mwili na magonjwa kama saratani, ini na ukosefu wa lishe na inapunguza rehamu na kutibu presha.

Mmea wa Rosella wenye maua mekundu hujulikana kama choya-Dodoma, huitwa mkakaka (pwani) na wengine huutumia kama kiungo cha mbog (ndimu). Majani yake yanaweza kuliwa kama mboga vilevile ni zao la biashara na hutumiwa nyumbani.

Aina  Za  Rozela
Kuna aina 2  za Rozela
i. : – Hibiscus sabdariffa yenye vikonyo vya rangi nyekundu hadi njano ambavyo vinaliwa
ii. Hibiscus altissima Webster ambayo hupandwa zaidi kwa ajili ya kamba kamba (fibres) zake lakini vikonyo haviliwi.

Mahitaji ya Mrosela
Hali ya Hewa:
Maeneo ya tropiki yenye mvua kati ya 1500 – 2000 mm kwa mwaka,Mwinuko wa hadi meta 600 kutoka usawa wa bahari na Inavumilia joto na hali ya unyevunyevu

Aina ya udongo wa kulima Rosella
Rosella hupendelea udongo wa mchanga wenye rutuba ambao hupenyeka kwa urahisi, Hata hivyo unaweza kukua kwenye aina mbalimbali za udongo na huhitaji palizi ya mara kwa mara ili kuondoa kivuli na majani pia huvumilia mafuriko, upepo mkali na maji yaliyotuama

Ulimaji wa Rozela
Uchaguzi wa eneo, utayarishaji wa eneo, uchaguzi wa mbegu
• Mahitaji ya bustani : vikapu, mbolea, udongo, mchanga
• Tifua ardhi vizuri kwenda chini kama sentimeta 20
• Piga mashimo ya ukubwa wa sm15 X sm 15 na kina cha sm 5
• Panda mbegu kilo 11 – 22 kwa hekta
• Ni vyema kupanda mbegu kwa mistari
• Palizi katika mwezi wa kwanza ni muhimu sana
• Mbolea za asili zinafaa kutumika na husaidia sana
• Mtindo wa kubadilisha mazao (crop rotation) hutumika hasa kwa ajili ya mdudu anayeshambulia mmea huu kwenye mizizi (root knot nematode) Heleredera radicicola
• Unaweza kubadilisha na mazao ya kijani kama kunde, mahindi
• Mashamba madogo nyumbani: – Panda mistari halafu ikisha ota punguza iwe katika mistari ya meta 1 x meta 1.
• Mashamba makubwa: – Mbegu zioteshwe kwenye kitalu halafu zipandwe shambani kwa upana wa meta1.3 hadi 2.6 na mistari ya upana wa meta 2-3.3 Magonjwa • Fungi: fangas (ukungu) mbalimbali hushambulia kwenye mizizi na majani – Nyunyiza dawa, fungicides Kumbuka: Uangalizi wa shamba unahusisha; – Palizi, Kukata mapukutu, kufyeka – Kunyweshea – Uwekaji mbolea – Uwekaji dawa kwa wadudu waharibifu

Uvunaji wa Rozela
Uvunaji wa matunda na vikonyo hufanyika majuma 3 baada ya maua kuchipua, wataalamu wanashaui vikonyo viondolewe baada ya kupika matunda

•Kwa Rosela ya kamba: kupanda hadi kuvuna ni miezi 3-4 na ivunwe wakati mimea inatoa maua –
Mimea ikatwe chini kabisa na kisha kuning’iniza ili kamba ziachane na mti – Kamba zioshwe na kuanikwa juani – Mashine zipo na zinaweza kutumika kwa ajili ya kutenganisha kamba na mti • Ukaushaji Unafanywa kwa kutumia – solar dryer – chekecheke – Kuanika moja kwa moja juani – Kutumia majamvi kwa kukaushia matunda yenye mbegu

Maandalizi:
Anza kwa kuandaa turubai, jamvi, mkeka, baada ya hapo bandua vikonyo.Alafu hifadhi matunda yenye mbegu na Weka rosela iliyokauka kweye mifuko safi ya nailoni au viroba ukimaliza Hifadhi mifuko kwenye chumba kisafi chenye mzunguko mzuri wa hewa na kisiwe chenye unyevunyevu

Uvunaji wa kiuchumi
• Uvunaji wa vikonyo kilo 1.5-7.5 kwa mmea
• Kilo 17000-19000 kwa hekta
• Uzalishaji wa kamba ni kg 1700 – 3500 kwa hekta
• Kiasi cha kamba kwenye rosela ni 5%
Matumizi ya Rosela – Majani, matunda, maua, vikonyo, mbegu, mizizi
i. Vikonyo vya matunda hutumika kutengenezea jams, jellies, sauces na mvinyo
ii.Vikonyo pia hutumika kuweka rangi na ladha kwenye vyakula
iii.Majani machanga huliwa kama mboga
iv. Mbegu hutumika kwa ajili ya kuongeza nguvu za kiume
v.Matunda yake yanaliwa
vi.Kamba zake hutengenezea vitu mbali mbali
vii.Rosela pia hutoa mafuta
viii.Inatumika kutengeneza mvinyo mzuri  sana.

Matumizi Ya  Rozela kama dawa asilia
Hupunguza kiwango cha kulewa kwa mtu anapokunywa pombe
Huongeza nguvu za kiume
- Maua yake ni mazuri sana katika kupunguza lehemu ( Kolestrol ) kwenye damu.
-Hutibu magonjwa ya tumbo, majipu, matatizo ya moyo, kikohozi, kansa (vikonyo), homa homa, na magonjwa ya akili