FAHAMU KUHUSU NAMNA YA KUTHIBITISHWA KWA AJILI YA UFUGAJI NYUKI NA MAZAO YA PORINI

Share:
Je unahitaji kujua nini kuhusu uthibitisho wa mazao ya porini na ufugaji nyuki?
- Shughuli za Ukusanyaji wa Mazao ya Porini na Ufugaji Nyuki zinaweza kuthibitishwa kulingana na viwango vya kilimo-hai vilivyopo. Shughuli hizi zifanyike kulingana na viwango na kuthibitishwa na mamlaka ya uthibitisho.

Shughuli za ukusanyaji wa mazao pori na ufugaji nyuki zinapaswa kufanywa bila ya kuharibu mazingira na zisitumie viambato ambavyo si vya asilia kama vile kemikali zisizoruhusiwa.

Vitu vinavyothibitishwa katika Ukusanyaji wa Mazao ya Porini?
Mazao yanayoota porini na mali ghafi zinazotoka porini: ikiwemo maeneo ya kukusanyia na shughuli nyingine zozote zinazofanyika baada ya ukusanyaji.

Mifano ya mazao ya porini:
- Uyoga
- Mkeka
- Vikapu
- Asili
- Kokwa
- Miti shamba
- Chavua

Uthibitisho pia utahusisha wabia wote wanaoshughulika na ukusanyaji wa mazao pori:
. Wamiliki wa ardhi au mameneja
. Wakusanyaji mazao au wakala wa maeneo
. Wasindikaji
. Anayeendesha mashine za kusindika mazao pori

Wabia hawa wanatakiwa wapewe mikataba na kutaarifiwa kuhusu sheria za ukusanyaji mazao pori

Je unahitaji nini ili uweze kuthibitishwa kwa Ukusanyaji wa Mazao Pori
Shughuli za ukusanyaji wa mazao pori zifanyike kulingana na viwango vya kilimo-hai.

Shughuli hizi zinajumuisha:
- Ainisha na weka mipaka maeneo ya ukusanyaji wa mazao pori. Mazao yasikusanywe kutoka maeneo ambayo kemikali zisizoruhusiwa zinatumika

- Usitumie mbinu za ukusanyaji ambazo huharibu mazingira

- Toa mafunzo kwa wakusanyaji wote kuhusu mbinu bora za ukusanyaji

- Weka kumbukumbu ya mazao yaliyokusanywa

Angalizo: Epuka kukusanya mazao kutoka maeneo ya hifadhi au spishi zilizokatazwa

Vitu vinavyothibitishwa katika Ufugaji Nyuki
Mazao ya nyuki yanayotokana na shughuli za ufugaji nyuki shambani

Kwa mfano:
- Asali
- Chavua
- Nta

Uthibitisho utahusisha maeneo yafuatayo:
. Vyanzo vya makundi ya nyuki na nta
. Maeneo wanapokula nyuki na hifadhi yao
. Kuvuna mazao ya nyuki na hifadhi yao
. Kusindika mazao ya nyuki
. Kumbukumbu za ufugaji nyuki
. Mmiliki na wafugaji wengine shambani

Kwa habari zaidi kuhusu ufugaji nyuki kwa viwango vya kilimo-hai na uthibitisho, wasiliana na Shirika la Taifa la Kukuza na kuenbdeleza Kilimo hai (NOAM) katika nchi yako.

Unawezaje Kuthibitishwa
Wakusanyaji wa mazao pori na wafugaji wa nyuki wanaweza kutafuta uthibitisho kupitia hatua zifuatazo.

Katika mwaka wa Kwanza:
Hatua 1: Soma habari kuhusu viwango na habari nyingine kutoka Shirika lako la Taifa la Kilimo-hai.

Hatua 2: Ulizia habari kutoka katika mamlaka za Uthibitisho zilizopo. Wasiliana na Mamlaka na upate habari husika kuhusu viwango, mchakato wa maombi, gharama za uthibitisho, na taratibu.

Hatua 3: Chagua Mamlaka ya Uthibitisho inayofaa. Jaza na wasilisha maombi, jadiliana nao gharama za uthibitisho, taratibu na malipo ya ada. weka saini mkataba wa ukaguzi na uthibitisho na Mamlaka hiyo.

Hatua 4: Ukaguzi panga na mamlaka ya Uthibitisho lini mkaguzi atakuja kukagua shughuli za ukusanyaji wa mazao pori na ufugaji nyuki na kumbukumbu. Mtu mmoja atafuatana na kumsaidia mkaguzi wakati wote.

Hatua 5: Jadili ripoti ya ukaguzi na Mkaguzi. Soma ripoti kwa uangalifu na kagua iwapo ina makosa yoyote au haieleweki.

Hatua 6: Jibu maswali yote kutoka kwa mkaguzi. Kagua na timiza mashati yote yanayohitajika kwa ajili ya uthibitisho wako.

Hatua 7: Uamuzi wa uthibitisho. Mamlaka ya uthibitisho hatimaye itakutaarifu matokeo ya ukaguzi na uamuzi wa uthibitisho.

Wawezaje kuendeleza uthibitisho
Shughuli za ukusanyaji wa mazao pori na ufugaji nyuki zitakaguliwa kila mwaka na Mamlaka ya Uthibitisho. Hahakikisha masharti yote ya uthibitisho kutoka kwenye Mamlaka ya Uthibitisho yanatimizwa.

Kwa hiyo, unapaswa kufanya yafuatayo:
- Fanya marekebisho yaliyoagizwa, wakati viwango vikibadilishwa
- Weka kumbukumbu zako vizuri ziwe na taarifa za sasa
- Hudhuria mafunzo kuhusu usindikaji unaozingatia viwango vya kilimo-hai ili kuboresha maarifa yako
- Linda maeneo ya mazao pori na ufugaji nyuki yasichafuliwe na viambato visivyo asilia

Huu ni mwongozo wa msingi wa msingi wa jinsi mkulima anavyoweza kuthibitishwa. Kwa habari zaidi wasiliana na Shirikisho lako la Kilimo-hai katika anuani zifuatazo

Tanzania Organic Agriculture Movement
TOAM
P.O BOX 70089, Dar es salaam, Tanzania
Tel: 255 732 975 799
toam@kilimohai.org
www.kilimohai.org

Burundi Organic Agriculture Movement
BOAM
P.O BOX 2251, Bujumbura- Burundi
Tell: 257 79910345
sinbad53@gmail.com

NOGAMU
P.O BOX 70071, kampala, Uganda.
Tell: 256 312 264039
admin@nogamu.org.ug
www.nogamu.org.ug

KOAN
P.O BOX 72461-00200, Nairobi, Kenya
Tel: 254 20 2610863
Email: koansecretariat@elci.org
www.koan.co.ke

ROAM
B.P 6886 Kigalli- Rwanda
Tel 250 788558027
Email: rwandaorganicmovement@gmail.com

IFOAM
International Federation Organic Agriculture Movements
Tell- 49 228 92650 10
Email:headoffice@ifoam.org
www.ifoam.org