Na George Mandepo, Mwanasheria, kitengo cha Sheria Wizara ya kilimo, Chakula na Ushiika
Aina mbali mbali za rasimali mimea kwa ajili ya chakula na kilimo ni malighafi wa maumbile ya mazao, iwe kwa wakulima wenyewe kuchagua, kuzipanga katika mafungu aina za mbegu au kwa kutumia teknolojia za kisasa za kuzalisha mbegu chotara, ni muhimu katika kukabiliana na mabadiliko yasiyotabirika ya mazingira na mahitaji ya baadaye ya binadamu.
Ujuzi wa asili kuhusu matumizi na utendaji kazi wa rasilimali za kibaolojia na asili imesaidia kuendeleza mamilioni ya mazao ya chakula cha wakulima wanayotumia sasa, pamoja na utajiri mkubwa na madawa ya mitishamba yanayosaidia kilimo endelevu na matumizi bora ya rasilimali. Ujuzi wa asili umechukua nafasi kubwa katika uhifadhi wa rasilimali za kijenetikia na uenezaji wa asilimali hizo kwa makampuni ya mbegu, wazalishaji wa mimea na taasisi za utafiti. Kwa bahati mbaya, ujuzi huu wa asili umekuwa ukitoweka kwa kasi kubwa. Hali hii ni tishio kwa haki miliki na uchumi wa mchakato wa utandawazi ambao umekuwa ukidhoofisha maisha ya asili ya kijijini.
Haki za kuhifadhi, kutumia, kubadilishana na kuuza mbegu za kilimo zilizohifadhiwa na matokeo, na kushiriki katika kufanya maamuzi kuhusu matumizi ya rasilimali za kijenetikia kwa ajili ya chakula na kilimo. Ni muhimu haki za wakulima zikatambulika na kukuzwa katika ngazi ya kitaifa na kimataifa.
Ili kuweza kugawana kwa usawa matunda ya mchango wao wa aina mbali mbali za rasilimali mbegu na ujuzi wa asili, jumuiya ya kimataifa imeridhia mikataba miwili ya umoja wa Mataifa ambayo itabania kisheria- Mkataba wa Kusimamia tofauti za Kibiolojia wa Mimea (CBD) na Mkataba wa Kimataifa wa Rasilimali mbali mbali za mimea ya Chakula na kilimo (ITPGRFA), iliyopitishwa November 3, 2001 chini ya mwavuli wa FAO.
Mikataba hii inatambua mchango mkubwa wa wakulima na jamii zao katika kuendelea kuhifadhi na kuendeleza rasilimali mimea ya asilia. Pamoja na Mkataba wa CBD kuzitaka nchi zilizoridhia kuheshimu, kuhifadhi na kudumisha ujuzi wa asili, ubunifu na uzoefu, na kuhimiza ujuzi wa asili, ubunifu na uzoefu, na kuhimiza haki na usawa katika kugawana faida inayotokana na matumizi ya rasilimali mimea katika ngazi ya kimataifa, imeonekana kuna haja kubwa ya kuboresha mfumo wa kisheria ili kulinda ujuzi wa asili na haki za jamii ya wakulima.
Ili kulinda haki za watafiti, wagunduzi au wabunifu wa aina za mimea mipya, serikali ya Tanzania ilitunga sheria Na. 9 ya Haki za Wazalishaji mimea mipya mwaka 2012, sheria ambayo inashabihiana na sheria ya UPOV ya mwaka 1991. Wakati Haki za Wazalishaji mimea mipya hulinda haki za wakulima kupanda mbegu siyo haki ya kunufaika kutokana na mbegu za mimea nayo siyo haki miliki kwa mujibu wa PBR
Sheria mpya inayosimamia haki za jamii ya wakulima inahitaji kutungwa katika ngazi ya kitaifa kwa mujibu wa mikataba wa kimataifa wa rasilimali za kijinetikia ya mimea kwa ajili ya chakula na kilimo (ITPGRFA). Dhana ya kugawana faida ilivyoainishwa ndani ya ITPGRFA Tanzania kupitishiwa ndani ya ITPGRFA Tanzania kupitishiwa nchini, inasema wakulima ambao watakaochangia kutoa vipindikizi vya mbegu watatambulika na kupewa marupurupu kisheria.
Mapendekezo ya mkataba huo yatawezesha Tanzania kutimiza majukumu yake ya kimataifa ya kuhifadhi na kuendeleza matumizi ya rasilimali mimea kwa ajili ya chakula na kilimo na ulinzi wa haki za wakulima husika. Sheria hiyo mpya itawezesha utekelezaji wa ulinzi wa haki za wakulima katika ngazi ya kitaifa, ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa ulinzi wa ujuzi wa asili kuhusu rasilimali ya mimea kwa ajili ya kilimo na chakula; haki sawa ya kugawana faida itokanayo n amatumizi ya rasilimali ya mimea kwa ajili ya kilimo na chakula; haki sawa ya kugawana faida itokanayo na matumizi ya rasilimali mbegu; na haki ya kushiriki katika kufanya maamuzi ngazi y akitaifa kuhusiana na mambo ya uhifadhi na matumizi endelevu ya rasilimali za kijinetikia katika chakula na kilimo.