SHUGHULI ZA USINDIKAJI ZINAWEZA KUTHIBITISHWA KUWA NI ZA VIWANGO VYA KILIMO HAI

Share:
1. Unahitaji kujua nini kuhusu usindikaji wa mazao ya kilimo-hai
Shughuli za usindikaji zinaweza kuthibitishwa kulingangana na viwango vya kilimo-hai vilivyopo. Hii hutokea pale shughuli hizi zinapotimiza masharti ya viwango na kuthibitishwa na mamlaka ya uthibitisho.

Kwa nini ni muhimu?
- Kumsaidia msindikaji kupata masoko ya bidhaa za kilimo-hai
- Kuonyesha kwamba shughuli za usindikaji haziharibu mazingira
- Kuonyesha kwamba wafanyakazi wanatendewa vyema
- Kutoa taarifa kwa wateja kwamba bidhaa inatokana na kilimo-hai na chanzo kinafahamika

2. Shughuli gani za usindikaji zinaweza kuthibitishwa kama ni za kilimo-hai
Shughuli zozote zinazofanywa kuhusiana na mazao baada ya kuvunwa kuanzia uchanganyaji wa kawaida hadi shughuli za usindikaji unaotumia mashine.

Uthibitisho utahusisha maeneo yafuatayo:
- Chanzo cha mali ghafi
- Chanzo cha visiadizi vya usindikaji, viambato na viungo vya nyongeza
- Kuweka vitambulishi vya bidhaa wakati wa usindikaji
- Kumbukumbu za usindikaji na hifadhi ghalani
- Kumbukumbu za manunuzi na mauzo
- Vifaa vya usindikaji
- Wafanyakazi wa usindikaji
- Wasindikaji wa mkataba

3. Unawezaje Kuthibitishwa
Ili aweze kuthibitishwa, msindikaji atahitajika kutimiza hatua zifuatazo.

Katika Mwaka wa Kwanza:
Hatua 1:
Soma habari kuhusu viwango na habari nyingine kutoka Shirika lako la Taifa la Kilimo-hai

Hatua 2:
Ulizia habari kutoka katika Mamlaka za Uthibitisho zilizopo. Wasiliana na Mamlaka na upate habari husika kuhusu viwango, mchakato wa maombi, gharama za uthibitisho, na taratibu.

Hatua 3:
Chagua Mamlaka ya Uthibitisho inayofaa. Jaza na wasilisha maombi, jadiliana nao gharama za uthibitisho, taratibu na malipo ya ada. Weka saini mkataba wa ukaguzi na uthibitisho na Mamlaka hiyo.

Hatua 4:
Ukaguzi wa usindikaji. Panga na Mamlaka ya Uthibitisho lini mkaguzi atakuja kukagua shughuli za usindikaji na kumbukumbu. Mfanyakazi mmoja aliyechaguliwa atafuatana na kumsaidia mkaguzi wakati wote.

Hatua 5:
Jadili ripoti ya ukaguzi na Mkaguzi. Soma ripoti kwa uangalifu na kagua iwapo ina makosa yoyote au haieleweki.

Hatua 6:
Jibu maswali yote kutoka kwa mkaguzi. Kagua na timiza masharti yote yanayohitajika kwa ajili ya uthibitisho wako

Hatua 7:
Uamuzi wa uthibitisho. Mamlaka ya uthibitisho hatimaye itakutaarifu matokeo ya ukaguzi na uamuzi wa uthibitisho.

4. Unawezaje Kuendeleza Uthibitisho wako
Shughuli za usindikaji zitakaguliwa kila mwaka na Mamlaka ya Uthibitisho. Msindikaji ahakikishe masharti yote ya uthibitisho kutoka kwenye Mamlaka ya Uthibisho yanatimizwa

Kwa hiyo, unapaswa kufanya yafuatayo:
- Fanya marekebisho yaliyoagizwa, wakati viwango vikibadilishwa
- Hudhuria mafunzo kuhusu usindikaji unaozingatia viwango vya kilimo-hai ili kuboresha maarifa yako
- Weka kumbukumbu zako vizuri ziwe na taarifa za sasa
- Linda mazao ya kilimo- hai yasichafuliwe na viambato visivyo asilia

Huu ni mwongozo wa msingi wa jinsi mkulima anavyoweza kuthibitishwa. kwa habari zaidi wasiliana na Shirika lako la kilimo-hai katika anuani zifuatazo:

TOAM
P.O BOX 70089, Dar es salaam, Tanzania
Tel: 255 732 975 799
E-mail: toam@kilimohai.org
www.kilimohai.org

BOAM
P.rO BOX 2251, Bujumbu- Burundi
Tel: 25779910345
E-mail: sinbad53@gmail.com

NOGAMU
P.O BOX 70071, Kampala, Uganda.
Tel: 256 312 264039
admin@nogamu.org.ug
www.nogamu.org.ug

KOAN
P.O BOX 72461-00200 Nairobi, Kenya
Tel: 254 20 2610863
E-mail: koansecretariat@elci.org
www.koan.co,ke

ROAM
B.P 6886 Kigali-Rwanda
Tel: 250 788558027
E-mail: rwandaorganicmovement@gmail.com

IFOAM
Tell: 49 228 92650 10
E-mail:headoffice@ifoam.org
www.ifoam.org