TOFAUTI KATI YA MBEGU ZA ASILI, CHOTARA NA MBEGU ZENYE VIINI TETE

Share:

By Abdallah Ramadhani Mkindi, Mratibu, TABIO

Mbegu ni pembejeo muhimu sana katika uzalishaji wowote wa kilimo. Katika kilimo, mbegu ni chanzo cha nafaka na mbegu nyingine za siku zijazo.

Hapo zamani mbegu zikipatikana bure kwa wakulima wengi na wakulima  na uwezo wa kuhifadhi na kubadilishana miongoni mwao Hivyo ilikuwa siyo rahisi kutenganisha, utamaduni na ujuzi wa jamii husika. Kadiri miaka ilivyopita, wakulima walianza kushauriwa kutumia mbegu zilizotengenezwa na taasisi za utafiti wa kilimo kwa madai ya kuongeza mavuno na kudhibiti magonjwa. Matokeo yake ni kwamba , biashara ya uzalishaji wa mbegu ukaanza kuchukua nafasi kubwa na wanasayansi na makampuni ya biashara ya uzalishaji wa mbegu ukaanza kuchukua nafasi kubwa na wanasayansi na makampuni ya biashara walianza kuwekeza zaidi maarifa na mitaji yao katika uzalishaji mbegu. Mbegu zinaweza kugawanywa katika makundi matatu, mbegu za asili, mbegu chotara na mbegu zenye viini tete.

Mbegu za asili ni zile ambazo wakulima wametumia katika maeneo yao ya kilimo kwa vizazi vingi. Kwa kawaida mbegu hizi mwenekano wa kijinetikia. Mbegu kama hizi hali ya maumbile ya eneo husika, kibiolojia na mazingira husika. Kwa maelfu ya miaka, vizazi vya  wakulima Tanzania na kote duniani wamekuwa wakichunguza mbegu, chagua, kuzikuza, kuzalisha na kuzitunza ili kuweza kuende;eza ukulima kutoka kizazi kimoja hadi kingine. kwa kupanda na kutunza makundi ya aina za mbegu, wakulima wameweza kutengeneza wigo wa ulinzi wa kilimo chao na kujihakikishia mavuno-hata kama mvua zimechelewa au imewahi, ukame umepita, mafuruko yakaja, wadudu na magonjwa yakawepo. Ujuzi wa kina wakulima na uwelewa wao wa mazao wanayopanda, uchaguzi makini na mbegu na hali ya mazingira wanamoishi vimewasaidia wakulima kujiwekea hazina ya vyanzo vya mbegu ambamo wanaweza kuendeleza uzalishaji.

Ujuzi huo unawezesha kuzalisha mbegu zaidi zenye kustahimili na zenye kustahimili na zenye lishe bora. Hata hivyo mbegu za asili zinatishwa sana na ukame, kukosekana mavuno kutokana na ukame, mazingira mabaya ya utunzaji, umaskini na uboreshaji wa kilimo ambapo wakulima wameendelea kununua mbegu. changamoto nyingine ni kuzuka kwa makampuni yanayoingia katika sekta ya mbegu huku seikali ikiendelea kujitoa katika kusaidia kuimarisha mifumo ya ndani ya uzalishaji mbegu na kuacha kusaidia kuzuia upotevu wa mbegu za asili.

Mbegu chotara ni mbegu zinazozalishwa kwa kupandisha mbegu mbili zinazotokana na wazazi tofauti kijenetikia. Taaluma ya kutengeneza mbegu chotara inafanyika kwa kuzuia mwingiliano wa mbelewele za mimea na wakati mwingine chotara hutokea yenyewe. Uzao wa mimea hiyo miwili tofauti huzaa aina mpya ya mmea wenye tabia kutoka kwa wazazi mpya ya mmea wenye tabia kutoka  kwa wazazi wawili. Uzao mpya unaweza kuongezewa uchotara tena kwa ajili ya kuongeza mavuno, lishe, utamu au uvumilivu katika mazingira. Mbegu cotara hazitunziki kwani hazina uwezo wa kuzaa chipukizi sahihi, kwa hiyo uzao wao huwa haufanani moja kwa moja na wazazi. Mbegu chotara lazima zinunuliwe kila mwaka,  hivyo hongezea mkulima hali tegemezi kwa kampuni za watengenezaji wa mbegu. Mbegu chotara zinahitaji mbolea nyingi za viwandani na hii hufanya mbegu hizi kupendwa na wadudu.

Ongezeko la matumizi ya madawa ya kuulia wadudu huleta magonjwa na hata maafa kwa binadamu, wanyama na wadudu wengine wenye manufaa. Matumizi ya madawa na mbolea za viwandani yakizidi huondoa mbolea ya asili iliyopo katika udongo. Madawa na mbolea za chumvi chumvi hutiririshwa na maji kuingia katika mito na hatimaye kupelekea uharibifu wa naji na viumbe vya majini.

Mbegu za viini tete au GMO ni mimea au wanyama ambao wametengenezwa kutokana na kupandikizwa vinasaba (gene) kwa kutumia teknolojia ya vinasaba. Teknolojia hii huunganisha vinasaba au DNA kutoka familia mbali mbali za mimea na kutengeneza muunganiko dhaifu wa mimea, wanyama, bakteria na vinasaba vya virusi ambavyo visingeweza kuzaliwa katika hali ya kawaida au kwa njia ya asili ya upandikizaji mbegu. Kitendo cha wanasayansi kufanikiwa kuingiza vinasabandani ya mbegu kimewafanya wajidai eti  wametengeneza kitu kipya . Mkulima anapopanda mazao ya viini tete, hufanya hivyo kwa idhini iliyotengenezwa  na kumiliki haki ya mbegu hizo. Idhini hii hulipiwa kupitia ongezeko la bei ya mbegu atakayolipa mkulima. Wakulima hawaruhusiwi kuhifadhi mbegu hizi kwa ajili ya kupanda msimu ujao kwa vile mbegu ni mali ya kampuni hizo. Au kwa upande wa mazao mengine kama soya ambayo yanaweza kutunzwa na kupandwa msimu unaofuata, mkulima hulazimika  kulipia leseni kwa kampuni ili aruhusiwe kupanda mbegu hizo kwa maraya pili, na asipofanya hivyo atakuwa hatarini kushtikiwa mahakamani.

 Hii ndiyo sababu mbegu za viini tete ni ghali zaidi kuliko mbegu chotara na ni sababu hiyo  inayofanya makampuni makubwa ya kimataifa kujaribu kadiri iwezekanavyo kuwaingiza wakulima katika mfumo wa kutegemea mbegu za viinitete. Ukweli ni kwamba kwa viwango vyote, mbegu hizi za viinitete siyo bora kuliko mbegu za asili zilizopo kwa wakulima. Mazao yake hutokana na mbegu chotara ambazo zimewewa viinitete, na siyo kutokana na uandishi wenyewe wa viinitete.

 Si kweli kwamba GMO huongeza uzalishaji.  kwa ajili yake, mbegu za viinitete haipendi kilimo cha mseto, na hivyo haiwezi kustahimili magonjwa na wadudu . Ni aina mbili tu ya mazao ya viinitete imeshaingizwa katika biashara, nayo ni ile yenye madawa ya magugu na ile inayostahimili sumu itokanayo na Bt. Mazao ya viinitete yenye madawa ya magugu huaminika kuweza kujikinga na madhara ya magugu wakati ile ya Bt ina uwezo wa kujikinga na wadudu.

Kwa kuthibitisha, mbegu ni uhai na yeyote anayesh mbegu anashikilia uhai. Tukiangalia ina hizo tatu za mbegu zilioelezewa hapo juu, ni zile mbegu za asili tu ndizo zimebaki mikononi mwa mkulima. Hali hii inapelekea kuwepo na haja ya kusaidia jitihada za kuzitambua na kufufua mbegu za asili ambazo zinataka kupotea.