Fahamu kuhusu homa ya matumbo ya kuku na namna ya kutibu

Share:
Ugonjwa huu husababishwa na bacteria na huwapata kuku wa umri wote. Mara nyingi ugonjwa huu huambukizwa kutoka kwa kuku wagonjwa kwenda kwa kuku wasio wagonjwa kupitia kwenye mayai , chakula chenye kinyesi cha kuku wenye ugonjwa pia watu iwapo watabeba vimelea na kuja navyo kwenye banda.

Jinsi unavyoambukiza:
Vyakula vya kuku kutoka sehemu yenye ugonjwa kwenda kusiko na ugonjwa.
Kuku asiye mgonjwa kula vimelea vya ugonjwa kupitia kinyesi cha kuku mgonjwa kwenye chakula.
 Mizoga ya kuku yenye ugonjwa ikipelekwa sehem isiyo na ugonjwa.
Kuku mgonjwa huweza kurithisha vifaranga wake kupitia mayai yaliyotagwa.
Watu na vyombo vya usafiri wanaweza kuhamisha ugonjwa kutoka sehem hadi sehemu.

Dalili za ugonjwa huu ni;
Homa Kali
Kinyesi kuonekana kuganda sehem za nyuma.
 Kiwango cha utagaji hushuka.
Manyoya husimama
 Kuku kudhoofika
Kukosa hamu ya kula.

Kinga:
Tenganisha vifaranga na kuku wakubwa.Kuku wagonjwa watengwe na kupewa tiba ya antibiotic.Zingatia usafi wa banda na vyombo vya chakula na maji.