Takribani zaidi ya miaka 200 iliyopita, rais wa kwanza wa marekani George Washington aliwahi kusema: "Ni janga kwa mkulima kulazimika kununua mbegu zake. Kubadilishana mbegu inaweza kuwa ya manufaa fulani, lakini kuzinunua baada ya kulima msimu wa kwanza ni kuvunjiana heshima". Maneno yake yanatufundisha kuwa wakulima wakati ule kimsingi walijitosheleza na walinunua tu mbegu za kutosha mwanzo wa kuanza kulima. Lakini sasa yote haya yamebadilika. Sasa 98 ya wakulima nchini Maekani hununua mbegu kila mwaka kutoka kwa makampuni ya biashara ya mbegu.
Kwa mujibu wa muungano wa mapinduzi ya kijani kibichi Africa (AGRA), 90% ya wakulima Tanzania hupata mbegu zao kutokana na mfumo wao wa asili wa kutunza mbegu. Wanatunza mbegu kutokana na mavuno ya msimu uliopita au wanabadilishana na kununua mbegu kutoka kwa wakulima wengine kijijini. Ni 10% tu ya wakulima wanapata mbegu zao kutoka makampuni rasmi ya biashara za mbegu.
WATUNZAJI WA BAIOANUWAI
Kwa maelfu ya miaka, viazi vya wakulima kote duniani wamekuwa wakichunguza na kuchagua, kutunza, kuzalisha na kuhifadhi mbegu ili kila kizazi kijacho kinakuwa na aina mbalimbali za mbegu. Wakulima mara nyingi wametumia ubunifu wao kulima mazao aina mbalimbali ili kukabiliana na changamoto nyingi za udongo, tabia nchi, lishe ladha, uhifadhi, wadudu na magonjwa. ni Afrika wanawake wametoa mchango mkubwa katika jamii zao kwa kazi yao ya kuwa watunzaji wa mbegu.
Karne iliyopita imeshuhudia kushuka kwa kasi idadi na aina za mbegu duniani, hasa baada ya makampuni makubwa kuanza kujiingiza katika sekta ya mbegu. Makampuni haya yanalenga kutengeneza kundi lingine la wateja wao wa mbegu kutoka miongoni wa mabilioni ya wakulima ulimwenguni, kiasi kwamba kwa sasa makampuni matatu makubwa ndiyo yanayodhibiti soko la mbegu duniani. Haki za wakulima kutunza, kuzalisha, kubadilishana na kuuza mbegu zimeanza kudhoofika kwani sheria za nchi nyingi zimekuwa zikitoa upendeleo kwa makampuni ya kibiashara njia za asili za wakulima kufanya kazi zao.
Taarifa ya Shirika la kilimo cha Chakula Duniani (FAO) iliyochapishwa 2010 inakisia kuwa 75% ya mazao yote yameshatoweka duniani. Mmomonyoko wa rasilimali baioanuwai za kilimo unaendelea. ujuzi wa mbegu za asili hazirithishwi tena kwa vizazi vijavyo, kwani wakulima huhimiza au hulazimishwa kununua mbegu.
Kuhama kutoka mbegu za asili zinazolimwa kwa zinazolimwa kwa ajili ya virutubisho, kwenda kuzalisha aina chache tu za mazaoya chakula kingi, yamechangia kupotea kwa virutubisho na lishe kamili. Hii imesababisha kuwepo hali ya utapiamlo. Bei ndogo ya mazao ya chakula katika soko la dunia tafsiri yake ni kwamba wakulima wengi wanajikuta wakiwa na madeni makubwa ya malisho ya mifugo, nishati mimea na mazao ya biashara ya nyuzi. Pamoja na shinikizo hili nina imani kwamba kilimo cha mashamba makubwa kina tija kuliko cha asili, wakulima wa mashamba madogo.