MCHANGO WA OXFAM KATIKA KUKABILIANA NA UHABA WA CHAKULA
By Shija Msikula, Mshauri sekta binafsi, Oxfam
Oxfam Tanzania inajishughulisha na Haki ya Kiuchumi ili kuboresha maisha ya wakulima wadogo vijijini, wafugaji na kwa mkazo wa kipekee ustawi wa wanawake. Haki ya kijinsia-kwa maana ya kufutilia mbali hali ya manyanyaso kwa mwanamke , kugawana mali sawa na kupata fursa ya uongozi na kushiriki kama raia jasiri na muhimu katika jamii. KwaOxfam, ubora wa elimu na uwezeshaji jamii ni nyenzo muhimu itakayowasha mabadiliko ya maisha ya jamii zilizobaguliwa.
Kazi ya Oxfam katika sekta ya kilimo Tanzania hivi karibuni imezingatia kuleta mabadiliko ya mfumo wa masoko kwa njia ya kuanzisha minyororo ya thamani ya sekta ndogo kama vile: mnyooro wa mboga na soko lake mkoani Tanga; huku wa kienyeji, mafizeti na masoko yake mikoani Morogoro na Dodoma; na mifumo ya soko la mifugo wilaya ya Ngorongoro.
Kwa kutumia ushirikiano katika mnyororo wa thamani wakulima wadogo wanapata fursa ya kutumia mazao yao kufanya biashara.
Mikakati na shughuli za Oxfam zinapangwa na kutekelezwa kwa kushirikiana na jamii, halmashauri za wilaya, asasi zisizo za kiserekali na sekta binafsi. Kupitia ushirikiano huo, shirika limepata uzoefu unaoweza kuleta mabadiliko ya kijamii na kiuchumi katika ngazi mbalimbali, kushawishi mabadiliko ya sera na kuwaunganisha watu na vyanzo vya rasilimali za ndani na nje ya nchi. Lengo ni kuboresha wazalishaji wadogo wa kilimo, kuongeza mapato kutokana na uwekezaji, kukuza biashara za mazao ya kilimo na kuboresha viwanda vya usindikaji na uuzaji ili kutengeneza mazingira ambapo watu wanaoishi katika hali duni wanaweza kuuza kile wanachozalisha.
Ushirikiano kati ya Oxfam na shirika lisilo la kiserikali liitwalo Lushoto Business Technology Incubation Centre (LBTIC) tangu mwaka 2010 umelenga katika kuimarisha uwezo wa kikundi hiki cha uzalishaji na kuwawezesha kujua tabia na mienendo ya vikundi, ujasiriamali na mbinu bora za kilimo kama njia ya kufanikisha kutambua mifumo ya soko la mboga. Mwaka 2011, Oxfam ilianzisha ushirikiano mwingine wa HomeVeg, kampuni ya kitanzania inayomilikiwa na watu binafsi. HomeVeg ina uzoefu mkubwa wa kilimo cha mboga zenye thamnani ya juu, uwezo wa kimataifa wa kuendesha kilimo kizuri na kuwajengea wengine uwezo huku ikiuza mboga katika masoko ya Ulaya. HomeVeg hufanya kazi kwa njia ya kilimo cha mkataba kati yake na vikundi vya wazalishaji.
Kimsingi miradi kadhaa inatekelezwa Tanga, ikiwa ni pamoja na ile ya miaka mitatu (2012 - 2015) ya mnyororo wa kuongeza thamani na mboga unaofadhiliwa na Scotland. Katika mradi huu, wakulima wa mboga wamejipanga katika vikundi. Vikundi hivyo vinaratibiwa na umoja wa wakulima wa lushoto-Korogwe Vegetable (LUKOVEG). Usanifu wa mradi ulitumia mfumo wa ujasiriamali na masoko unaozingatia uswa wa kijinsia (GEM) ili kutoa fursa ya uchambuzi wa kina wa masuala ya kijinsia, nafasi ya wanawake kusimamia uchumi na mabadiliko ya tabia ya nchi katika mfumo wa masoko. Mradi huu unalenga wazalishaji wadogo wa mboga 4500 katika Mkoa wa Tanga na utagusa moja kwa moja maisha ya wakulima wengine wa mboga wapatao 10,000. Hadi sasa kuna vikundi 57 vya uzalishaji na wazalishaji 2,596 ambapo kati yao 1,592 ni wanawake.
UPATIKANAJI WA FEDHA
Wakulima wa mboga hupata mtaji kwa ajili ya kilimo kupitia mfuko wa vikundi vyao uitwao VICOBA na Vyama vya Ushirika ya Akiba na Mikopo (SACCOS). Jumla ya VICOBA 48 vimeanzishwa, 16 kati yao wanapata huduma kutoka SACCOS ya UATAMIZI ambayo huwasaidia kupata mikopo kwa uraihisi kutoka NMB lushoto. Wakulima wa njegere kwa ajili ya soko la nje hupata mitaji kutokana na mkataba kati ya pride RFW na HomeVeg ambapo riba ni 2% kwa kila mzunguko wa miezi minne. "Tuna vikundi vipya 20 ambavyo vimeunganishwa na SACCOS ili wajifunze na kujengwa zaidi". Anabaini mmoja wa viongozi wa SACCOS.
UHUSIANO NA SOKO LA NJE
HomeVeg inafanya kazi kwa kufuata misingi ya soko kwanza ambapo wakulima wanawezeshwa kwa utaratibu wa GAP kuweza kuzalisha mboga ya viwango vizuri zinzokidhi viwango vya kusafirishwa kwenda soko la nje. wakulima wote wanaozalisha mazao bora zaidi wameunganishwa na masoko ya Ulaya kupitia HomeVeg. Mara baada ya kuvuna, wakulima huuza mavuno yao kwa HomeVeg. Kampuni huweka mboga katika jokofu kabla ya kusafirisha kwenda ambapo uchambuaji na ukaguzi hufanyika kasha kufungwa katika vifurushi vya ukubwa unaokubalika. Wakati wa mavuno ya msimu wa mwaka 2012.13, wakulima wa njegere wapatao 605 walipeleka nje jumla ya kilo 51,773 na kupokea TZS 87,542,745. Wakulima sasa wanaweza kuzalisha ka 200 kwa sanduku la kilo 10 kwa ajili ya kupata kibali cha kusafirisha mazao, kodi ya TRA inayokusanywa katika Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro.
Mradi huu ni miongoni mwa miradi iliyofanikiwa sana. Kuna uhakika wa soko la Umoja wa Ulaya, bei nzuri ipo na wanunuzi wa kuaminika wapo na hivi ndivyo siri ya mafanikio ya mradi huu wa mboga. HomeVeg imefaulu kufikia viwango vya ubora vya soko la Umoja wa Ulaya, japokuwa uzalishaji bado uko chini ya kiwango cha mahitaji ya soko. Kampuni inatakiwa kuuza tani 100 za njegere kwa wiki lakini uwezo wa sasa ni tani 10 kwa wiki. Mpango wa HomeVeg wa kuendesha kilimo cha mkataba umevutia wakulima wengi kushiriki katika uzalishaji mboga. Faida ya kilimo cha mkataba ni kwamba wakulima wanafahamu mnunuzi ni nani, kiasi kinachotakiwa kuzalishwa na bei ya kuuzia hata kabla ya kuotesha mboga. Faida ya kilimo cha mkataba ni kwamba wakulima wanafahamu mnunuzi ni nani, kiasi kinachotakiwa kuzalishwa na bei ya kuuzia hata kabla ya kuotesha mboga. Wakulima hupata huduma za ugani. Sababu nyingine ni uhusiano mzuri kati ya washirika wa maendeleo na serikali. Pamoja na mafanikio, baadhi ya changamoto zinajitokeza, kuanzia zile ambazo hazitabiriki hadi hali hewa isiyoeleweka pamoja na ufahamu mdogo wa wananchi. Utaratibu wa kilimo cha mkataba bado ni mgeni kwa wakulima wengi. Baadhi ya wakulima hawafuati masharti ya kilimo yatakayowezesha uzalishaji wenye tija. Changamoto nyingine ni ugumu wa kupata mikopo kutoka taasisi za fedha, ukosefu wa vyombo vya usafiri kwa ajili ya maafisa ugani kuweza kutembelea maeneo yao ya kazi, bila kusahau utaratibu mgumu wa ukusanyaji kodi.