Kazi ya mboji
Kuongeza rutuba ardhini. Chembechembe za udongo ardhini ni mchanganyiko maalum wa mchanga, tope na mfinyanzi ulioshikamanishwa na mboji. Hulifanya umbo la udongo kuwa bora zaidi.
Mboji ikiwa haba:
Mchanga , tope na mfinyanzi havishikamanishwi vema. Mvua ikinyesha hapo, matone huuhaibu udongo huo kwa uahisi sana. Nafasi ile inayotokea kati ya chembe moja na nyingine huwa haipo tena. Chembechembe hugandamana na kuwa ngumu. Umbo la udongo huo huwa baya.
Mboji ikiwa nyingi shambani:
Mchanga, tope na mfinyanzi hushikamana kwa njia ifaayo. Hivyo chembechembe zinazotokea baada ya kutifua ardhi na kuulainisha udongo vema, haziharibiwi na matone ya mvua. Umbo la udongo hubakia kuwa zuri. Mizizi husambaa na kukua vema. mmea hulishwa ipasavyo kwa hiyo, tukitaka kulifanya umbo la udongo lipendeze zaidi, yatupasa kuongeza rutuba ardhini.
Katika sehemu hii ya pili, tutajifunza Njia mbalimbali za kuongezea udongo rutuba. Ili udongo uwe na rutuba na mboji, ni muhimu kupumzisha shamba lako.
Pia ukiacha Mboji Unaweza pia kurudishia udongo rutuba ukitumia baadhi ya njia zifuatazo:
- Kutumia mabua na masalia ya mazao
- Kutumia nyasi na majani
- Kutumia samadi
- Kutumia mbolea ya mchanganyiko (mboji)
- Kutumia udongo wa zizini
Wakati unapotifua, takataka hizi huchanganyika na udongo, huozeshwa na kuwa virutubisho na mboji, hivyo kuongeza udongo rutuba.
Pia zipo njia nyingine za kilimo bora zinazosaidia kuurutubisha udongo.
- kilimo cha mzunguko wa mazao
- Kutumia mbolea ya kijani
- Kilimo mseto
Tuzingatie njia hizo za kurutubisho udongo upate kuchagua na kuzifuata zile zinzokufaa wewe.