USINDIKAJI WA KOROSHO KWA ASILIMIA 100 KUTOKA TANZANIA: INAWEZEKANA

Share:

Na Mwandishi wa ANSAF
Hata hivyo, viwango vya Mpango Maendeleo wa umoja wa Mataifa (UNDP) huweka Tanzania miongoni mwa nchi zenye  "maendeleo duni ya binadamu". Kwa mujibu wa kigezo cha UNDP cha maendeleo ya binadamu, Tanzania ilishika nafasi ya 152 kati ya nchi 1987 duniani kote mwaka 2013. Umaskini ni tatizo Tanzania, na huonekana zaidi vijijini. Umaskini wa vijijini una mahusiano makubwa na kilimo. Pamoja na ukuaji wa idadi ya watu kwa wastanik wa 3%, uchumi wa Tanzania umeimarika katika kipindi cha miongo miwili iliyopita, huku pato la taifa (GDP) ikikuwa kwa wastani wa 7%. Ukuwaji wa pato la taifa  (GDP) kati ya mwaka 1988 na 2012 ulikuwa ni wa wastani wa dola za marekani 341 (TZS 545,600). Wakulima wadogo ndio wadau wakuu katika suala la uhakika wa chakula na huzalisha sehemu kubwa ya malighafi zinazohitajika katika viwanda vya kusindika mazao msingi na nyongeza.

Wakati uchumi wa Tanzania umeendelea kutegemea kilimo, kumekuwa na jitihada za serikali na wadau wengine muhimu kuunga mkono mipango ya kuboresha kilimo na kuleta mapindazi katika sekta unaonyesha fursa kubwa zilizopo katika minyororo mbalimbali ya thamnani, kwa njia ambazo wakulima wadogo wanaweza kunufaika, na kuchangia uchumi wa kitaifa kwa kutengeneza ajira. Pia ni dhahii kuwa kiwango cha ukosefu wa ajira ni kikubwa, na wahitimu wa vyuo wanahitaji ajira zitakazowahakikishia maisha bora. Korosho ni miongoni mwa mazao asilia yanayosafirishwa nje ya nchi na kuleta fedha za kigeni. Ni miongoni mwa mazao makuu matatu yanayosafirishwa nje ya nchi. Katika miaka ya awali baada ya uhuru, Tanzania ilikuwa ikizalisha asilimia 20% ya koosho yote kimataifa na ilizalisha wastani wa metric tani 145,000 mwaka 1974. Sekta hii ndogo ya korosho ilikumbana na changamoto nyingi zilizosababisha kudorora kwa uzalishaji kwa takriban miongo mitatu na nusu. Mnamo mwaka 2012, Tanzania ilishika nafasi ya tatu Afrika na nafasi ya tatu Afrika na nafasi ya nane duniani kwa uzalishaji wa korosho. makamu wa Rais wa Tanzania Dk. Gharib Bilal aliwaambia washiriki wa mkutano wa sekta ya koosho kwamba ukuaji wa uchumi wa Tanzania  unategemea sana kilimo. "korosho ni zao muhimu katika hadhi yake ya kuleta maendeleo ya kiuchumi Tanzania" alisisitiza.

Katika kipindi cha miaka 15 iliyopita, uzalishaji wa korosho umekuwa ukiongezeka kwa kasi, na kufikia rekodi ya metric tani 158,000 mwaka 2012. Ongezeko hili katika  uzalishaji unakuja wakati uhitaji wa korosho asilimia 9-11% kwa miongo ijayo. Inakadiriwa kuwa, kwa idadi ya sasa ya miti ya korosho iliyopo na usimazi mzuri ukiwepobasi, wakulima Tanzania wanaweza kuzalisha hadi metric tani 300,000 kwa mwaka. Tanzania ina nafasi kubwa ya kunufaika na fursa zilizopo katika zao la korosho katika ngazi ya kitaifa na ya mtu binafsi. Hii ni kwa vile korosho inaweza kustawi katika wilaya nyingi Tanzania. kwa sasa kuna wilaya zaidi ya 40 zinazozalisha zao korosho kwa viwango tofauti. Tanzania inajivunia wataalamu wazuri katika moja ya taasisi bora za utafiti wa korosho-naliendele-katika nchi za Afrika kusini mwa jangwa lka Sahara. pia misimu huwezesha korosho ya Tanzania kustawi zaidi ukilinganisha na nchi nyingine za Afrika.

Uuuzaji wa korosho ya Tanzania kwa kiasi kikubwa umekuwa ni ule usiyobanguliwa, na wakulima wadogo ambao ndio watendaji wakuu husubiri kupangiwa bei. Hivi karibuni, serikali imeanzisha mfumo wa manunuzi kupitia stakabidhi ghalani. Kabla ya hapo bei ya shambani ilikuwa ndogo na uuzaji kwa ujumla ulikuwa holela na ulighubikwa na utaratibu mbovu. Kwa sasa, soko la korosho limeimarika na mfumo wa wachuuzi uliyopo umewavutia wanunuzi zaidi kuliko hapo, awali.Pamoja na mabadiliko hayo chanya, uwezo wa kusindika korosho Tanzania bado mdogo, na si zaidi ya asilimia 10% ya kile kiasi kinachozalishwa, huku India ikiendelea kubaki soko pekee inayopokea asilimia 90% ya korosho yote isiyobanguliwa

NINI MATOKEO YAKE?
Inakadiriwa kuwa katika kipindi cha miaka mitano (2008-2012), Tanzania imepoteza zaidi ya dola za Marekani milioni 750 (TZS 1.2 bilioni) kutokana na kusafirisha korosho ghafi kwendqa nje, na kwa wastani Tanzania imekuwa ikipoteza dola za Marekani 110 (TZS 176,000) kila mwaka, na kupoteza zaidi ya fursa za ajira 45,000 katika kipindi hicho. "Tanzania inahitaji fedha taslim na ajira kwa vijana wanao endelea kuongezeka. Mapato yaliyopotea yangeweza kuwekezwa katika maeneo mahususi ya kimkakati ya kukuza uchumi", anasemaAudax Rukonge ambaye ni Katibu Mtendaji wa ANSAF.

Kwa sasa mfumo wa usindikaji uliyoanzishwa hauwezi kukidhi viwango vya sasa na makadirio ya uzalishaji. Kuna haja ya kuwekeza katika mfumo bora wa viwanda vya kubangua korosho na kuwahakikishia wateja juu ya usalama wa chakula wanachonunua; hatimaye kuchangia ufanikishaji wa upatikinaji wa mapato mazui kwa wakulima wadogo.

ANSAF na Baraza la Kilimo Tanzania (ACT) kwa kushirikiana na Bodi ya korosho Tanzania (TIC) waliandaa mkutano wa kwanza wa wawekezaji wa korosho nchini Tanzania (TIC) waliandaa mkutano wa kwanza wa wawekezaji wa korosho nchini Tanzania uliofanyika katika kituo cha Mikutano ya Kimataifa cha Julius Nyerere, Dr es salaa, November 4 hadi 5, 2013. Mkutano uliwaweka pamoja wawekezaji wa ndani na nje nchi, watendaji wa sekta binafsi, taasisi za fedha, maafisa wa serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali na wakulima wadogo.

Lengo lilikuwa kujenga ushirikiano endelevu na kuibua fursa zilizopo za kuwekeza katika sekta ndogo ya korosho. Kwa mujibu wa waandaaji wanne wa mkutano huo, lengo kuu lilikuwa kurudisha zao la korosho katika nafasi yake halali kwa kutambua mchango wake katika uchumi wa nchi, ajira na kipato cha mtu binafsi kwa kuvutia wawekezaji watakaowezesha kuongeza uwezo wa kusindika korosho kwa asilimia100%