FAHAMU KUHUSU MAJI ARDHINI NA HEWA ARDHINI

Share:

Maji Ardhini
Maji ni muhimu sana katika udongo kwa kuwezesha viumbe hai kuendelea kuishi na kufanikisha kuoza kwa takataka. Maji huyeyusha virutubisho (chumvichumvi) ambapo vinyweleo vya mizizi ya mimea hunyonya myeyuko huo kama chakula.

Maji yanayoingia katika udongo, yanatokana na mvua na kumwagilia. Mvua inaponyesha, sehemu kubwa ya maji hutiririka na kuingia mtoni. Lakini sehemu nyingine hupenya ardhini.

Jinsi ya kuyasaidia maji kupenya ardhini
* Kwa kuufanya udongo kuwa na umbo zuri,
- kutifua ardhi vizuri kwa wakati ufaao.
- Kuongeza rutuba ardhini kila mara.

* Kwa kupambana na mmomonyoko wa ardhi
- Kufunika udongo kwa nyasi au mimea.
- Kulima shamba kwa kukingama mwinuko.
- Kulima matuta na kuchimba mitaro katika mstari wa usawa wa mwinuko.
- Kujenga mikandaa ya udongo au ya mawe ukifuata mistari ya uswa wa mwinuko

Hewa Ardhini
Hewa ni muhimu kama vile ilivyo maji kwa mimea mizizi ikikosa hewa haitaweza kunyonya chakula cha mmea.

Maji yasiwe mengi mno katika tabaka ya juu ya udongo unaolimwa kwani yatazuia hewa kuingia ardhini.

Mizizi ikikosa hewa, hufa.
Haiwezi kuupatia mmea chakula chake tena kwa hiyo hata mmea huo hufa.

Viini/vijidudu vilivyoko ardhini hihitaji hewa.
Viini na vijidudu viishivyo ardhini visipopata hewa haviwezi kupumua hatimaye hufa.

Hata hali ya kuoza kw anyasi hupungua au kusimama kabisa.

Hewa ikikosekana ardhini viini viharibifu huongezeka haraka na kuharibu chumvichumvi. Mimea hukosa chakula chake. Hivyo mavuno hupungua.

Minyoo nao huhitaji hewa ili waishi.
Ukitaka hewa iingie ardhini ushughulikie udongo wako kwa kuutifua vizui ndipo hewa itapenya ndani kwa urahisi na kuupa udongo la kupendeza