JUA ZAIDI KUHUSU MSETO WA MAZAO NA MITI

Share:
Huu ni mtindo wa kilimo ambamo miti mikubwa na midogo hungizwa katika mfumo mmoja na mazao, na hivyo kuoteshwa katika shamba moja. Miti hupandikizwa ama pembezoni mwa shamba ili kuonyesha mipaka, au ndani ya shamba kwa nafasi maalum, au hupandikizwa katika kanda mbaimbali ili kuleta kivuli kwa baadhi ya mazao.

Faida ya mtindo huu wa kulima ni:-
i. Baadhi ya miti kama Lukina hurutubisha udongo kutokana na naitrojeni inayotengenezwa katika mizizi yake.

ii. Migunga, mikwaju na Kavilea hurutubisha udongo kutokana na majani yake yanapodondoka na kuoza chini yake. Kutokana na rutuba hii. Mazao mbalimbali huweza kustawi vizuri chini ya miti hii.

iii. Pia husaidia kudhibiti mmomonyoko wa udongo

Angalia:
Mbolea za chumvichumvi, mbolea za viwandani zinazouzwa kwenye maduka ya kilimo haziongezi rutuba shambani. Lakini zimejaa chumvichumvi.

Chumvichumvi hizi haziupi udongo umbo la kupendeza kwa kuwa hazina mboji. Haziwezi kulingana na samadi au mbolea ya mchanganyiko, au kupumzisha ardhi