KUTIFUA UDONGO HUSAIDIA KUDUMISHA RUTUBA
Kutifua ni kupindua na kuvunja uso wa ardhi. Kupindua udongo huufungulia udongo vipenyo. Maji na hewa vitaweza kupenya na kuingia ndani kwa urahisi. Kutifua huwezesha viini na vijidudu kuishi vema ardhini.
Umbo la udongo huwa zuri na la kupendeza zaidi. Udongo wenye umbo zuri hustawisha mmea vizuri zaidi.
YALIYOMO KWENYE UDONGO
Ndani ya udongo kuna viumbe vingi, Vikubwa na vidogo visivyoonekana kwa macho tu. Pia kuna hewa, maji, n.k.
Kuna mimea na wanyama.
Wanyama ni kama vile minyoo na wadudu kama minyoo ya ardhini, konokono, tandu, jongoo, nchwa, siafu na wengine wengi.
Viini vidogo ni pamoja na bakteria, ukungu nyungumea na virusi.
Viini au vijidudu
Baadhi ya vijidudu husaidia kuozesha viumbe vilivyokufa na kugeuka mboji pia chumvichumvi. Baadhi ya viini hivi huharibu mbolea za chumvichumvi ardhini. Hivyo inadhihirisha kwamba vipo viini vyenye faida na hasara.
Viini vyenye faida huhitaji hewa: Viini vyenye hasara havihitaji hewa. Unapotifua shamba lako vizuri viini hivyo vyenye faida hufaidika kupata hewa.