KWA NINI UFUGAJI WA SUNGURA?

Share:
Watu wengi katika sehemu mbalimbali za Tanzania hawaoni umuhimu wa kufuga sungura, la sivyo sungura wanapatiana kwa kuwinda porini. Kwa hiyo inafaa kueleza sababu ya kufuga sungura:

i. Watu wanafuga sungura kwa kupata nyama, ngozi, sufu (mbegu ya Angora) na samadi.

ii. Ladha ya nyama ni nzuri. Nyama yake hulingana na nyama ya kuku.

iii. Nyama ya sungura huliwa na watu wa dini mbalimbali.

iv. Ufugaji wa sungura hauhitaji fedha nyingi.

v. Watu waishio katika nchi za tropiki wanatumia wanyama kama rasilimali yao. Wanapohitaji fedha kidogo ni rahisi kuuza mnyama mdogo kuliko kukata "mguu wa mbuzi".

vi. Wingi wa nyama unaopatikana kwa sungura hutosha kwa familia bila kuweka akiba (jokofuni)

vii. Dume moja na jike wawili wanatosha kuanza ufugaji wa sungura na wanahitaji nafasi ndogo.

viii. Malisho kwa wanyama hawa hupatikana kwa gharama ndogo.

ix. Sungura ni rahisi kushughulikiwa na wanawake na watoto pia.

x. Samadi ya sungura hutumika katika bustani na wanyama hawa hawana kelele.

Baada ya kueleza sababu ya kufuga sungura, lazima tuangalie pia matatizo yake:

i. Kuanza kufuga sungura (gharama kwa kujenga kizizi, kununua sungura na malisho yao) huhitaji fedha taslimu.

ii. Mfugaji akifuga sungura wengi, mara nyingi anahangaika kupata wateja.

iii. Sungura wanapata magonjwa kama wanyama wengine, lakini ni vigumu kupata matibabu.

iv. Kufuga sungura huhitaji muda kama kutunza sungura watano inachukua saa 1-2 kwa siku. Hii inatokana na kuwatunza wanyama hawa katika kizizi zhao tu.

Muhtasari:
Ufugaji wa sungura unafaa hasa kwa wakulima wadogo na wenye nia.

Idadi ya wanyama isizidi upatikanaji wa malisho na nafasi katika kizizi. Ni muhimu sana kupata wanyama wenye afya bora kwa kufuga.

Kumbuka: Kwanza kujenga kizizi, halafu wanyama!

Maelezo mafupi kuhusu sungura wenyewe
Asili ya sungura wa kufugwa wametokana na wenzao wa asili huko Ureno, Hispania na Afrika ya Kaskazini. Toka hapo binadamu wamesambaza sungura katika sehemu mbalimbali ulimwenguni. Wakati wa Warumi watu wameanza kufuga wanyama hawa. Katika ulimwengu tunazo mbegu 100 aina mbalimbali na wenye rangi zaidi ya 200. Uzito wa sungura waliokomaa huhitiliafiana kadiri ya mbegu kilo 1-8