Kwa jamii zote za wanadamu, kitendo cha kuelimishana ni muhimu sana. Kwani huwafanya watu kupokezana maaifa ambayo yakitumiwa vizuri huleta maendeleo.
Maarifa yapo aina nyingi yanaweza kuwa ya kiuchumi, kijamii au kisiasa n.k. maarifa haya yana lengo la kustawisha hali ya maisha ya jamii inayohusika.
Wakulima pia wanahitaji kuelimishana au kupokezana maarifa ili waweze kuboresha kilimo na maisha yao kwa ujumla.
Ili kufanikisha jambo hili, wakulima wasitegemee sana wataalamu kuwafanyia au kuwaelekeza mambo yote kuhusu kilimo
Wao wenyewe wanaweza:
* Kuepeana ujuzi tofauti uliopo katika eneo lao kwa kutumia rasilimali zilizopo
* Kushirikishana mambo mapya yanayoibuka katika mazingira yao.
* Kuchukuliana matatizo kwa kupeana ushauri wa jinsi ya kuyatatua.
Hali hii ya wakulima kujifunza kupitia kwa wakulima wenzao wenye uzoefu mbali mbali katika kilimo na ufugaji ndio inayoitwa " Mafunzo kwa njia ya Mkulima kwa Mkulima".
Wakulima wote wanaoshiriki katika mafunzo haya hutoa mchango katika mafunzo kwa uwazi.
Hivyo, mafunzo ya mkulima kwa mkulima ni muhimu kwani yanawaondolea wakulima shida nyingi wanazozipata kwa kusubiri wataalamu ambao huenda wasipatikane wanapohitajika kutoa ushauri wa kutatua matatizo yao.
Aina za wakulima wanaotoa elimu au maarifa
Katika Mkulima kwa Mkulima kuna wakulima wanaojifunza na wakulima wanaotoa elimu kwa wenzao. Wakulima wanaotoa elimu wapo wa aina mbili.
Nao ni:
Wakulima Wabunifu na
Wakulima Washauri