NAMNA YA UJENZI WA VIZIZI VYA SUNGURA
Kuanzia magonjwa, kutokufuga jike na dume wa ukoo mmoja (Inbreed), kuzuia kupandwa jike mapema na kuwachinja sungura waliokomaa, inatakiwa kujenga kizizi au kitundu.
Maelekezo kabla ya kujenga kizizi
i. Mfugaji yampasa kujenga kitundu au kizizi imara hata kama angetumia gharama kubwa, lakini ujenzi huo utatu-mika kwa sungura wengi na kwa muda mrefu.
ii. Inashauriwa mwanzoni kujenga kizizi chenye ukubwa wa wastani, kuliko kujenga kizizi kikubwa kitakacholeta matatizo (kukosa ujuzi wa kufuga sungura).
iii. Kizizi kijengwe kwa mtindo wa kufaa, ili shughuli zifanyike kwa urahisi (kulisha, kusafisha na kushika mnyama).
VIPIMO VYA BOKSI (cage)
Vipimo vya boksi huhitilifiana na ukubwa wa mbegu ya sungura
Mbegu ya sungura Uzito wa mnyama Vipimo vya boksi (kwa cm)
aliyekomaa urefu Upana Kimo
- Heavy breed Kilo 5,5 - 7,0 120 x 80 x 60
(mkubwa)
- Medium breed Kilo 3,5 - 4,5 100 x 80 x 55
(wastani)
- Light breed Kilo 1,5 - 3,0 80 x 70 x 50
(mdogo)
Ramani ya kwanza: KITUNDU CHA MBEGU WASTANI
Kitundu hiki kimewekwa chini ya upenu wa nyumba fulani. Ukubwa huu (100x80x55 cm) unatosha kwa ufugaji wa jike, kuzaa pamoja na watoto hadi kumaliza kunyonya.
Maelezo ya namba katika ramani:
i. Nguzo za boksi (boriti).
ii. Sakafu ya lati. Katikati ya lati kuna nafasi ya sentimeta 1 juu na sentimeta 3 chini, kwa ajili ya kupitisha kinyesi na mkojo.
iii. Waya wa kufunga mbele.
iv. Kifuniko cha mlango.
(1) Mgawanyo katika kitundu (sectional view)
Kama inavyoonekana katika picha kifuniko cha kitundu kimetengenezwa kama mlango. Hii ni kwa sababu ya kurahisisha kazi ndani ya kitundu na wanyama hawawezi kuukia nje kwa urahisi.
Ramani ya pili: KITUNDU CHA SEHEMU MBILI
Kitundu hiki kina vipimo: urefu 200cm, upana 80cm, kimo 60cm. Nje kwa kila upande kuna nguzo mbili zenye urefu wa sentimeta 120. Kila sehemu inatosha kwa kufugia. Katikati pametengenezwa chombo kwa ajili ya malisho kama vile majani makavu (hay).
(2a) Kitundu chenye sehemu mbili (front view)
Maelezo ya namba katika ramani:
i. Mlango na waya
ii. Kitasa cha kufunga milango miwili
iii. Chombo cha malisho (hay n.k)
iv. Boksi la kuzalia (half open type nest box)
(2) Kitundu chenye sehemu mbili kinavyoonekana toka juu
Maelezo ya namba katika ramani:
i. Boksi la kuzalia
ii. Chombo cha malisho (nay n.k.)
iii. Sakafu ya lati
iv. Chombo cha maji
v. Chombo cha malisho (kama pumba)
vi. Mlango
Boksi la kuzalia
Makusudi ya boksi ni kumpa jike nafasi ya kutengeneza kiota chake. Boksi wazi (a) ni rahisi kwa kumudu na kutengeneza. Kinyume chake kiota huwa wazi. Katika boksi lililofungwa (c) kiota kimejificha kwa usalama, lakini ni vigumu kukimudu kwa matenenezo yake. Chini ya boksi kuwe na matundu ya kupitisha mkojo. Hapa kuna aina tatu za boksi.
Kizizi au kitundu kisinyeshewe mvua. Kwa hiyo, yafaa kupanda miti au vichaka kuzunguka kizizi. Miti inayofaa ni ya jamii ya kunde kama Lusina au Caliandra, kwa sababu majani yake hutumika kwa malisho. kitu muhimu kwa sungura ni hewa safi, hasa wakifungwa ndani ya nyumba. Kama kinyesi hukaa kwa muda mrefu bila kuondolewa, hewa ya Amonia huathiri sungura. Yafaa kuondoa kinyesi mara mbili kwa wiki na kuweka matandiko mapya chini ya vitundu, kwa mfano unga wa mbao.
Kwa ajili ya kutengeneza sakafu yafaa kutumia lati, mianzi, au waya ya pekee.
Faida nyingine ya kufuga sungura ni samadi yake, hasa kwa bustani. Ndani ya samadi kuna asilimia 0,8 naitrojeni, o,2 fosiforasi na 0,7 potassium. Sungura mmoja anatoa kilo 45 za kinyesi kwa mwaka. Pia anakojoa karibu gramu 400 kwa siku. Mfugaji akifuga sungura kumi, atapata mbolea ya kutosha kwa bustani