NAMNA YA ULISHAJI WA SUNGURA
Sungura hula wakati wote na anahitaji usiku na mchana kupata malisho ndani ya chumba chake. Kutwa hutafuna mara 80 malisho yake. Wanyama hawa vipande vya tumbo (appendix) vikubwa na ndani yake hutengeneza kinyesi cha pekee. Kinyesi hiki ni laini ambacho huliwa tena usiku, ili kupata vitamini B vya kutosha. Pia wanahitaji vitu vigumu ili kufupisha meno yao, kama matawi ya mforosadi (mulberry tree) au Calliandra na mlusina. Kuwalisha sungura malisho sungura malisho bora na ya kutosha huwafanya wakue upesi, wazae sana pia wawe na afya bora.
Malisho
Kila aina ya malisho huwa na maji na vitu vikavu kama vile protini, kutia nguvu na joto (carbonhydrate and starch), mafuta, kamba, madini na vitamini.
Wanyama hawa yafaa wapate malisho aina mbalimbali.
Malisho mabichi:
Nyasi (K.mf. Brachiaria), majani ya porini (K.mf Manyonyoli- black jack), marejea, nandala, komfrey, mchicha, majani ya karoti, chaina, kabichi, majani ya miti kama mlusina, mforosadi na Calliandra n.k.
Malisho yaletayo nguvu:
Pumba, mahindi, wali, ngano, mtama, viazi mviringo na vitamu, muhogo mtamu, matunda, ndizi, karoti, vipande vya mkate.
Malisho yenye kamba-kamba:
Nyasi kavu (hay) na majani makavu ya mpunga na ngano.
Madini:
Chumvi
Malisho ya pekee:
Mashudu na "broiler mash" (malisho ya kuku)
Malisho ya sungura lazima yaangaliwe sana yasiwe na udongo, uchafu, uozo na joto la kushindiliwa (majani mabichi). Kuongeza madini hasa kwa jike anayenyonyesha inabidi kuchanganya chumvi kijiko cha chai kimoja na kilo moja ya pumba. Nyasi kavu (hay) zisitumike mara baada ya matengenezo, walau kuongoja wiki sita hadi kulisha. Malisho mabichi yaliyolowa yasitumike mara moja kwa kulisha, yafaa yanyauke kidogo. Kabla ya kulisha inafaa kuondoa mabaki. Inashauriwa mfugaji asibadilishe malisho ya aina moja na kuweka mengine ghafla.
Kiasi gani na aina ipi ya malisho ambayo mnyama hupewa, hutegemeana na hali yake. Kwa mfano, jike anayenyonyesha anahitaji maisho yaletayi nguvu kwa wingi na watoto hukua upesi. Vilevile, huhitaji malisho mengi kuliko waliokomaa.
Maji ni muhimu sana kwa wanyama, lakini watu wengine wanafikiri sungura hawahitaji maji kwa malisho. Kumbuka, mwili hutoa daima maji kwa njia ya pumzi, mkojo, kinyesi pamoja na maziwa.
Mahitaji ya maji kwa kutwa:
Robo lita kwa sungura mkubwa.
Lita moja kwa jike anayenyonyeshwa hadi wiki tabu baada ya kuzaa
Lita mbili kwa jike anayenyonyesha toka wiki tatu hadi wiki sita.
Kuna vifaa mbalimbali vinavyotumika kwa kunyweshea maji.
a) Kopo au chungu
b) Chupa na koki au sahani
c) Kontena ya plastiki (lita 1) yenye koki (tazama picha uk. 19).
Vifaa vya na.
a) vioshwe kila siku kwa kuzuia ugonjwa wa Coccidiosis.