UBUNIFU: KUUA MAKORONGO NA KUYAGEUZA MASHAMBA YA KILIMO KWA KUTUMIA MAKINGA MAJI YA MAJANI NA MASALIA YA MATAWI YA MITI

Share:

Bw Raphael Chimolo ni mkulima mbunifu kutoka kijiji cha Chamkoroma Wilaya ya Kongwa Mkoa wa Dodoma. Ubunifunwake ni kuua makorongo na kuyageuza kuwa mashamba ya kilimo kwa kutumia makingamaji asili yaliyotengenezwa kwa kutumia majani na masalia ya matawi ya miti. Pia ni mtunza mazingira bora aliyewahi kupata tuzo za mtunza mazingira bora katika ngazi mbalimbali kuanzia ngazi ya kijiji mpaka taifa. Mkoa wa Dodoma hupata msimu mmoja wa mvua kwa wastani wa milimita 500 hadi 800 kwa mwaka.

 Hali ya hewa ni kame, yenye kipindi kirefu cha jua na mara nyingi hupata mvua chini ya kiwango cha wastani. Hali hii husababisha shughuli za kilimo kuwa ngumu, uzalishaji kuwa mdogo na matukio ya njaa kila mwaka kutokana na kutojitosheleza kwa chakula katika kaya. Kijiji cha Chamkoroma kimeathiriwa sana na mmonyoko wa ardhi na makorongo makubwa yanayosababishwa na hali ya asili ya udongo wa kiichanga, mvua zisizotabirika, na uharibifu wa mazingirifa unaotokana na shughuli mbalimbali za binadamu.

Lengo mahsusi la ubunifu
Kuongeza ukubwa wa shamba la kulima mazoa, kurutubisha udongo na kuongeza uzalishaji kwa kuua makorongo sugu na kuyageuza sehemu ya mashamba kwa ajili ya kupanda miti ya matunda, miwa, migomba, mahindi na mazao mengine ya kilimo.

Kilichomsukuma kuanza kubuni
Baada ya kumaliza elimu ya msingi, Bw. Chinolo alishindwa kuendelea na elimu ya sekondari kutokana na hali ya kiuchumi katika familia yake . Aliamua kwenda mjini kutafuta kazi lakini hakufanikiwa kama alivyotarajia. Baada ya kuona kwamba mjini hakukaliki, aliamua kurudi kijijini na kujiajiri katika shughuli za kilimo. Hata hivyo hakubahatika kupata shamba lililo bora kwa ajili ya kilimo. Alifunga safari kutoka kwao Kilosa kwenda Chamkoroma kutafuta shamba kwa ajili ya kilimo. Alibahatika kupewa shamba na serikali ya kijiji lakini shamba alilopewa lilikuwa katika sehemu ambayo imeshindikana kwa kilimo kutokana na makorongo makubwa yaliyokuwepo pamoja na ardhi yenye udongo uliochakaa kutokana na mmonyoko wa ardhi. Kwasababu alikuwa amedhamiria kupambana na changamoto hiyo, Bw. Chinolo hakukata tamaa. Alitafuta njia mbadala za kurudisha uhai wa shamba hilo kwa kutumia ubunifu wake. Alifanya jaribio lake kwa kuandaa makinga maji marefu ya majani yaliyochanganyikana na matawi ya miti ili aweze kuzuia mmonyoko wa ardhi kwa kupunguza kasi ya maji yanayotiririka kutoka katika milima inayozunguka kijiji hicho. Baada ya miaka michache jaribio lake lilifanikiwa kupunguza makali na ukubwa wa makorongo yaliyokuwepo kwa kiasi kikubwa, mazao yakastawi vizuri hatimaye mavuno yakaongezeka kutoka gunia 1la mahindi hadi 7 kwa eka ukilinganisha na awali. Mafanikio haya yalimpa nguvu ya kuongeza kasi ya kupanua ubunifu wake na kuhamasisha wakulima wengine kuanza kutumia ubunifu huo. Hadi kufikia mwaka 2007, Bw. Chinolo alikuwa ameshaanzisha vikundi vya wakulima zaidi ya 53 vinavyoshughulika na masuala ya kilimo, ufugaji na hifadhi ya mazingira.

Maelezo mafupi juu ya ubunifu huu

Kwanza kabisa katikati ya korongo, anaandaa kingamaji lenye mistari miwili (2) inayotokana na mambo za miti zilizopigiliwa kwenye udongo. Mambo hizo zinakuwa na urefu wa futi 4 kwenda juu kutoka usawa wa ardhi na upana wa futi mbili (2) kutoka mstari mmoja hadi mwingine. Baada ya kukomelea mabo hizo, anajaza majani ya kila aina, nyasi na masalia ya matawi ya miti katikati ya mambo hizo ili yaweze kupunguza kasi ya maji ya mvua kwa kuzuia mchanga, majani na takataka za kila aina zinazoletwa na maji ya mvua kwa kuzuia mchanga, majani na takataka za kila aina zinzoletwa na maji kutoka milima inayozunguka kijiji. Umbali kati ya kingamaji mojan ajingine ni mita 7 - 8 na idadi ya makinga maji kwenye korongo moja inategemea urefu wa korongo lenyewe. Kadri maji yanavyotiririka kutoka mlimani kupitia korongo, ndivyo mchanganyiko wa majani, takataka na mchanga vinavyotuama kwenye makingamaji, hivyo kutengeneza matuta katika korongo yanayotumiwa kupanda mazao ya kilimo kama miwa, migomba, magimbi, mashindi na miti mbalimbali ya matunda.

Faida alizozipata kutokana na bunifu hii ya kuuza makoongo
- Bw. Chinolo amefaniwa kuua makorongo yote katika shama lake na kuongeza ukubwa wa shamba analopanda mazao mbalimbali ya kilimo
- Amefanikiwa kurutubisha ardhi yake na kuongeza uzallishaji wa mazao kutoka gunia moja ya mahindi hadi saba (7) kwa eka moja, anajitosheleza kwa chakula, ameboresha mazingira yake kwa kupanda miti hivyo kujiongezea kipato kutokana na mauzo ya chakula cha ziada
- Ameweza kutumia ujuzi wake kuelimisha jamii juu ya kilimo bora, hifadhi ya mazingira na ushirikiano kupitia vikundi alivyoanzisha kijijini kwake
- Bw. Chinolo ni mkulima mkufunzi wa mfano anayetumiwa na wadau kadhaa wa mendeleo kuelimisha wakulima wenzake ndani na nje ya nchi na kujijenga jina.
- Ametunukiwa tuzo mbalimbali kwa kuwa mkulima na mtunzaji mazingira bora katika ngazi mbalimbali ikiwa ni pamoja na ngazi ya kijiji, wilaya, Mkoa mpaka taifa.