VIPENGELE VYA MSINGI KWA AJILI YA KUANZISHA BUSTANI
Uzalishaji wa mazao mengi na bora kunategemea sana maandalizi ikiwa ni pamoja na eneo, kitalu, upatikanaji wa maji, mbegu bora, mbolea, kuzuia magonjwa na kutumia teknolojia inayofaa.
Ili mkulima aweze kupata mazao mengi na bora hana budi kuzingatia mbinu zifuatazo:-
ENEO KWA AJILI YA BUSTANI
- Eneo lisiwe kwenye mteremko mkali kwa sababu sehemu kama hiyo inaweza kusababisha mmomonyoko wa udongo;
- Udongo usiwe wa mfinyanzi au wa kichanga. Udongo mzuri ni wenye rutuba na mboji nyingi au unaopitisha maji kwa urahisi;
- Eneo la bustani liwe karibu na chanzo cha maji cha kudumu; au kwenye maeneo ambayo hayana vyanzo vya maji vya kudumu, bustani iwe karibu ba kaya: maji ya kumwagilia yasiwe na chumvi chumvi nyingi kwani chumvi huathiri ukuaji wa mimea;
- Eneo la bustani au maziLUngira ya kayapandwe miti kwenye mipaka yake ili kuzuia upepo mkali. Upepo huufanya udongo wa juu kukauka haraka na kusababisha mmomonyoko wa udongo.
KUTAYARISHIA KITALU
- Kitalu kisiwekwe mahali penye kivuli kingi kwani kivuli husababisha mimea kukosa mwanga na hivyo kuwa dhaifu;
- Tifua udongo mwezi mmoja kabla ya kuotesha mbegu;
- Vunjavunja udongo ili kurahisisha upitishaji wa hewa na maji;
- Wakkati wa masika tengeneza matuta yaliyoinuka kkidogo ili maji yasituame;
- Wakati wa kiangazi tengeneza matuta yaliyodidimia kidogo ili kuhifadhi unyevunyevu
KUMWAGILIA MAJI
Hakikisha udongo una unyevunyevu wa kutosha kwa kumwagilia maji siku moja kabla ya kuotesha mbegu. Pia baada ya kupanda kitalu kimwagiliwe maji kidogo. Maji mengi huozesha mbegu.
KUPANDA MBEGU
- Tumia mbegu bora ambazo hazikushambuliwa na wadudu au wagonjwa;
- Nunua mbegu toka kwenye ofisi za kilimo, taasisi na maduka yanayoaminika;
- Panda mbegu ndogo kwenye kina kifupi na mbegu kubwa kwenye kina kirefu;
- Panda mbegu kila wiki ili kupata mboga mfulululizo.
MATUMIZI YA MBOLEA
Mboga hustawi vizuri kwenye udongo wenye rutuba. Kwa udongo usio na rutuba ni muhimu kuongezea mbolea ya samadi au mboji. Endapo uwezo wa kununua upo, mbolea za viwandani kama vile zile za chumvi chumvi; chokaa na kijivu zinaweza kutumika.
Mbolea za samadi au mboji ziwekwe kwenye bustani kabla ya kupanda mbegu au kupandikiza miche. Kiasi kinachotakiwa kuwekwa ni debe moja kwa tuta lenye upana na urefu wa mita moja. Mbolea za chokaa zitumike kwa kupandia mbegu au miche ya matunda na zile za chumvi chumvi zitumike kwa kukuzia mboga.
MGONJWA NA WADUDU WAHARIBIFU
Ni muhimu kukinga mimea dhidi ya wadudu na magonjwa ili kupata mazao mengi na bora. Zifuatazo ni njia mbali mbali zinazoweza kutumika katika kuzuia magonjwa na wadudu waharibifu.
UDHIBITI SANGO
Njia hii hutumia mbinu zifuatazo:
- Kupanda mbegu bora;
- Usafi wa bustani ambao ni pamoja na kuchoma takataka na kuondoa magugu yanayoweza kutunza wadudu na magonjwa;
-Kuchanganya mazao;
- Kutumia samadi na mboji
- Kupanda kwa nafasi
- Kutumia aina ya mbegu zinazovumilia au kustahimili mashambulizi ya magonjwa na wadudu.
UDHIBITI WA KITEKNOLOJIA
- Kutumia aina mnbali mbali za madawa;
- Kutumia mimea inayoua wadudu, kama vile muarobaini, pilipili kali, aina fulani ya maua: marejea, tumbaku, wadudu kama vile walawangi, manyigu na mbawakau.
KUMBUKA
- Mboga zilizonyunyiziwa dawa zitumike baada ya siku 14;
- Soma kwa uangalifu maelekezo ya matumizi ya dawa unayotumia;
- Pata ushauri toka kwa mtaalam wa kilimo.
VIFAA VYA BUSTANI
Ili kuboresha kilimo cha mboga na matunda ni muhimu kuwa na jembe, kamba, reki, uma wa bustani, ndoo ya kumwagilia maji, mboma la kunyunyizia dawa, toroli, panga, kiwanja, sepetu, beleshi, karai na kadhalika.
KUHIFADHI MBOGA NA MATUNDA
Mboga na matunda ni mazao yanayopatikana kwa msimu hasa sehemu zenye ukame. Mazao hayo huharibika pia haraka sana baada ya kuvunwa. Hivyo hivi ni muhimu kuhifadhi mboga na matunda ili upatikanaji wake kwa mwaka mzima.