Magonjwa ya kuku na tiba zake ni kama zifuatazo;
NDUI
YA KUKU (Fowl Pox)
Ugonjwa
huu husababishwa na virusi.
Dalili
za ugonjwa huu ni;
-Kuku
hupatwa na vidonda kichwani.
-Kuku
hupata uvimbe mweupe kwenye mdomo na kushindwa kula.
Tiba
za ugonjwa ndui
Ugonjwa
huu hauna tiba.
Kinga
za ugonjwa huu.
Chanja
kuku wako wa siku 60-90 kwa chanjo ya Ndui ya kuku (Fowl pox
vaccine).i.
GUMBORO
Ugonjwa
huu husababishwa na virusi.
Dalili
za ugonjwa
-Kuku
kuzubaa na kulundikana, pamoja na kusinzia
-Kuku
kuharisha
-Kuwa
na vifo vingi kwa kuku
Tiba.
Ugonjwa
huu hauna tiba,,Kuku wakipewa Dawa za oxytetracycline hupunguza vifo.
Kinga
wakinge kuku
wapo kwa kuwapa chanjo ya gumboro (Gumboro vaccine)
MDONDO
Ugonjwa
huu husababishwa na virusi
Dalili
za ugonjwa wa mdodndo
-Ugonjwa
huu hutokea kwa ghafla na kuenea kwa haraka
-Vifo
vya kuku huwa vingi
-kuku
hupumua kwa shida
-Kuku
hupooza na kulemaa miguu
-Kuku
hupinda shingo yake
-Kuku
hupunguza kutaga mayai
-kuku
huarisha
-Kuku
Kuzunguka zunguka na kutembea kinyume nyume.
Tiba
za ugonjwa za mdondo
Hauna
tiba
Kinga
za ugonjwa wa mdondo.
Chanja
vifaranga wako na kuku wako kwa chanjo ya Mdondo (New castle vaccine)
na urudie chanjo hii kila baada ya miezi mitatu.
MAHEPE
(Marecks)
Ugonjwa
huu husababishwa na virusi
Dalili
za ugonjwa.
-Kuku
hupata ulemavu na vifo vya mara kwa mara.
Tiba
za ugonjwa huu.
Ugonjwa
huu hauna tiba
Kinga
za ugonjwa huu.
Chanjo
hutolewa kwa vifaranga wenye umri wa siku moja,vifaranga hupewa
chanjo ya mahepe (Marecks vaccine)