UMUHIMU WA MKULIMA,MFUGAJI NA MFANYABIASHARA WA BIDHAA ZA KILIMO KUTEMBELEA MAONESHO YA WAKULIMA
Wakulima wengi hujisahau kwa kukusudia au kutokukusudia kwenda katika maonesho ya wakulima NANENANE ambayo hufanyika kila mwaka.Kimsingi maonesho haya ni muhimu kwetu wakulima na wafugaji na wafanyabiashara wa bidhaa za kilimo na mifugo.
Baadhi ya mambo muhimu ambayo mkulima, mfugaji au mfanyabiashara wa bidhaa za kilimo atayapata katika viwanja vya maonesho.
- Utapata fursa ya kuona mbegu bora za Mifugo ya aina mbalimbali Mpya na za zamani.
- Utakutana na watengenezaji wa Pembejeo na Zana mbalimbali za kilimo na kuona bidhaa zao kama vile zana mbalimbali za kilimo Kutoka SIDO,VYUO VIKUU,VETA,JKT,Na wadau wengine.
- Kupata elimu ya kilimo bora cha mazao mbalimbali ana kwa ana-Utakutana na wataalam na wakulima wazoefu mbalimbali ambao hutoa elimu bure kwa wakulima na pia hutoa uzoefu wao katika shughuli za kilimo.
- Utakutana na wajisiliamali wa mazao ya kilimo na mifugo na utajifunza mbinu mbalimbali za ujasiliamali kutoka kwao.
- Utakutana na wasindikaji wa mazao ya kilimo-hivyo utaweza kujifunza mbinu mbalimbali za uhifadhi,usindikaji,na ufungashaji wa bidhaa za kilimo.
- Utapata fursa ya kuziona na kuzitambua mbegu bora mpya na za zamani za mazao mbalimbali kutoka katika Taasisi za utafiti na wazalishaji mbegu wakishirikiana na Wakala wa Mbegu za serikali (ASA).