FAHAMU KUHUSU MAGONJWA YANAYOSHAMBULIA KAHAWA

Share:
Kilimo cha kahawa kimekuwa kikiwanufaisha kwa kiasi kikubwa wakulima ambao wanajihusisha na kilimo hicho ukiachana na faida wnayopata wakulima pia kuna changamoto magonjwa ammbayo inayowakabili wakulima hao

 Kuna magonjwa makuu ya manne ya kahawa ;
Chule buni (CBD)
- Kutu ya majani (Coffee leaf rust)
- Mnyauko fuzari (Fusarium) 

Kwa siku ya leo naomba tuangale ugonjwa wa chule buni 


CHULE BUNI (CBD- Coffee Berry Disease)
Chule Buni (CBD) ni ugonjwa wa matunda ya kahawa ambao umeenea sehemu nyingi nchini hasa zile za miinuko ya juu. Ugonjwa huu husababishwa na fangas wajulikanao kama colletotrichum kahawae. Ushambuliaji huwa ni mkubwa zaidi wakati wa mvua za masika kwani wakati huu hali ya unyevu unyevu kwenye hewa ni mkubwa na hali ya hewa ni ya baridi.


MADHARA
Ugonjwa huu huenea kwa kasi. Mbuni ulioshambuliwa haufi bali mkulima anaweza kupoteza mpaka asilimia 90 ya mavuno kwa mwaka kama hatazingatia namna bora ya kuuzuia.

Ugonjwa huu hushambulia mibuni katika hatua tatu muhimu nazo ni:
- Maua yanapochanua.
- Punje zikiwa changa na laini.
- Punje zinazoiva.

JINSI YA KUZUIA
Ili mkulima aweze kudhibiti vizuri ugonjwa huu anashauriwa:
- Kupunguza matawi yasiyotakiwa ili sumu iweze kupenya vizuri
na kufikia matunda yote.
- Kutumia sumu sahihi zilizopendekezwa kutumika kwenye kahawa.
- Kutumia kiasi na kipimo sahihi kilichopendekezwa.

Namna Kunyunyizia sumu wakati sahihi yaani:
- Kabla ya ugonjwa haujatokeza.
Unyunyuziaji dawa uanze wiki tatu kabla ya mvua za vuli kuanza (Oktoba - Novemba) na kurudiwa tena mwezi mmoja baadae (Disemba).
- Unyunyiziaji unaofuata ufanyike tena wiki tatu kabla ya mvua za masika (Machi) na kurudiwa kila mwezi hadi matunda yakomae (Julai).


FAIDA YA KUDHIBITI WADUDU WANAOSHAMBULIUA KAHAWA
- Atakuwa amepunguza uwezekano wa kuendelea kuongeza kasi ya huu ugonjwa mwaka hadi mwaka.
- Atakuwa ameongeza wingi na ubora wa kahawa.
- Atakuwa amejiongezea kipato chake na kuwa na maisha bora zaidi.
- Atakuwa ameongeza pato la taifa kwa ujumla.

MAMBO YA KUZINGATIA
Mwisho wa msimu hakikisha unaondoa matunda yote haswa yale yaliyoshambuliwa na chule buni.
- Tambua wakati sahihi wa kuzuia huu ugonjwa.
- Nunua sumu sahihi zilizopendekezwa.
- Hakikisha matunda yote yanapata sumu vizuri.
- Epuka ununuzi holela wa sumu kwani unaweza kununua hata zile zilizokwisha muda wake.
- Mara upatapo tatizo onana na mtaalamu wa kilimo/afisa ugani aliyekaribu nawe.